Connect with us

afyatips

Jinsi chumvi inavyoathiri mwili na kusababisha magonjwa

Avatar photo

Published

on

Jinsi chumvi inavyoathiri mwili na kusababisha magonjwa

Watu wamekuwa wakitumia chumvi tangu mwanzo wa ustaarabu wa kusindika, kuhifadhi na kuboresha chakula.

Katika Roma ya kale, chumvi ilikuwa muhimu sana kufanya biashara kiasi kwamba askari walilipwa mshahara wao, kwa mfano, kwa chumvi.

Thamani ya chumvi ilikuwa kwa kiasi fulani kama kihifadhi chakula, kudhibiti vijidudu visivyohitajika na kuruhusu vile vinavyohitajika kukua.

Ni uwezo huo wa ajabu wa kudhibiti ukuaji wa bakteria ambao huenda ulisaidia kukuza vyakula vilivyochacha kuanzia sauerkraut hadi salami, kutoka kwa zeituni hadi mkate, kutoka jibini hadi kimchi (mboga zilizotiwa chumvi na chachu).

Kuna ushahidi unaoongezeka kwamba chumvi nyingi (haswa kloridi ya sodiamu inayoongezwa ili kuhifadhi na kuongeza ladha ya vyakula vingi vilivyochakatwa) inawafanya watu kuwa wagonjwa.

Inaweza kusababisha shinikizo la damu na kuchangia mashambulizi ya moyo na kiharusi. Pia inahusishwa na ongezeko la hatari ya kupata saratani ya tumbo na koloni, ugonjwa wa Ménière(tatizo la sikio la ndani ambalo linaweza kusababisha kizunguzungu), mifupa na uzito uliokithiri.

Je, kitu kinachofikiriwa kuwa yenye thamani ya uzito wake katika dhahabu kinawezaje kubadilika na kuwa kitu ambacho taasisi nyingi za matibabu huzingatia kiashiria kikuu cha ugonjwa

Ushawishi wa chumvi unaweza kuwa jibu kwa swali hili.

Na kama mtaalamu wa magonjwa ya tumbo na mwanasayansi wa utafiti katika Chuo Kikuu cha Washington, ninataka kushiriki ushahidi unaokua kwamba vijidudu vilivyo ndani ya utumbo wako vinaweza pia kutoa mwanga juu ya jinsi chumvi inavyochangia magonjwa.

Shinikizo la damu

Jukumu la sodiamu katika shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo ni kwa kiasi kikubwa kwa sababu inadhibiti kiasi cha maji ndani ya mishipa ya damu.

Kwa maneno rahisi, zaidi ya sodiamu katika damu, maji zaidi huvutia ndani ya mishipa ya damu.

Hii husababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu na hatari ya kutokea mshtuko wa moyo na kiharusi.

Chumvi husababisha kupungua kwa vijidudu vyenye afya na metaboli muhimu wanazozalisha kutoka kwenye nyuzi.

Metaboli hizi hupunguza uvimbe kwenye mishipa ya damu na kuifanya itulie, ambayo husaidia kupunguza shinikizo la damu.

Isipokuwa kwa viumbe fulani ambavyo hustawi katika chumvi, inayoitwa halophiles, viwango vya juu vya chumvi vinaweza sumu karibu na vijidudu vyoyovyote, hata wale ambao mwili wako unavihitaji.

Ndiyo maana watu kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia chumvi kuhifadhi chakula na kuwaepusha na bakteria wasiohitajika.

Lakini mlo wa kisasa mara nyingi huwa na sodiamu nyingi. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, matumizi ya kiafya ni chini ya miligramu 2,000 kwa siku kwa mtu mzima wa wastani.

Wastani wa ulaji kimataifa wa miligramu 4,310 za sodiamu kuna uwezekano umeongeza kiwango cha chumvi kwenye utumbo juu ya viwango vya afya.

Chumvi katika uzito mkubwa

Sodiamu inahusishwa na matokeo mengine ya afya kando na shinikizo la damu, na microbiome yako inaweza kuwa na jukumu hapa pia.

Lishe ya juu ya sodiamu na viwango vya juu vya sodiamu kwenye kinyesi vinahusishwa kwa kiasi kikubwa na matatizo ya kimetaboliki, ikiwa ni pamoja na sukari ya juu ya damu, ugonjwa wa ini na kuongezeka kwa uzito.

Kwa kweli, uchunguzi mmoja ulikadiria kuwa kwa kila gramu ya ongezeko la kila siku la sodiamu ya lishe, kuna hatari ya kuongezeka kwa 15% ya uzito.

Utafiti wa kawaida wa lishe kutoka Taasisi za Kitaifa za Afya za Marekani uligundua kuwa wale waliofuata lishe ya vyakula vilivyosindikwa kwa wiki mbili walitumia kalori 500 zaidi na walikuwa na uzito wa kilo 1 zaidi ikilinganishwa na wale waliofuata lishe ndogo.

Moja ya tofauti kubwa kati ya milo hii miwili ilikuwa matumizi ya ziada ya gramu 1.2 za sodiamu na vyakula vilivyochakatwa zaidi.

Moja ya maelezo ni kwa nini kuongezeka kwa chumvi kunaweza kusababisha kupata uzito licha ya kutokuwa na kalori ni kwamba sodiamu huongeza matamanio.

Mataifa yanayopunguza matumizi ya chumvi

Wakati nchi nyingi zinatekeleza mipango ya kitaifa ya kupunguza chumvi, matumizi ya sodiamu katika sehemu nyingi za dunia yanaendelea kuongezeka.

Kupunguza chumvi ya lishe nchini Marekani haswa kunaendelea kudorora, wakati nchi nyingi za Ulaya zimeanza kuona faida kama vile shinikizo la damu na vifo vichache vinavyotokana na ugonjwa wa moyo kupitia mipango kama vile kuweka lebo ya chumvi kwenye vifurushi, urekebishaji wa chakula ili kupunguza chumvi. , na hata kodi ya chumvi.

Ulinganisho wa data ya lishe kwa bidhaa za chakula cha haraka kati ya nchi unaonesha tofauti kubwa.

Kwa mfano, kuku wa McDonald’s ni chumvi zaidi nchini Marekani na hata Coca-Cola ya Marekani ina chumvi, kiungo ambacho hakipo katika nchi nyingine.

Sekta ya chumvi nchini Marekani inaweza kuwa na jukumu katika suala hili.

Alisisitiza kuepuka kanuni za serikali kuhusu chumvi katika miaka ya 2010, tofauti na vile sekta ya tumbaku ilifanya na sigara katika miaka ya 1980.

Vyakula vyenye chumvi vinauzwa vizuri.

Mojawapo ya sauti kuu za tasnia ya chumvi kwa miaka mingi, Taasisi ya Chumvi ambayo sasa haifanyi kazi, inaweza kuwa imechanganya ujumbe wa afya ya umma kuhusu umuhimu wa kupunguza chumvi kwa kusisitiza hali ambazo hazijazoeleka sana ambapo kizuizi cha chumvi kinaweza kuwa hatari.

Lakini kuna ushahidi unaoongezeka wa haja ya kupunguza chumvi katika chakula, na taasisi zinajibu.

Mnamo 2021, Idara ya Kilimo ya Marekani ilitoa muongozo mpya ikitoa wito wa kupunguzwa kwa hiari polepole kwa chumvi katika vyakula vilivyotayarishwa kibiashara na kusindika.

Taasisi ya Chumvi ilivunjwa mwaka wa 2019. Mashirika mengine, kama vile Taasisi ya Vyakula Vilivyohifadhiwa Marekani na wasambazaji wakuu wa viambato, kama vile Cargill, wanakubali kupunguza chumvi kwenye lishe.

Uwiano sawa

Unawezaje kulisha vijidudu vya utumbo wako vizuri ukizingatia ulaji wako wa chumvi?

Anza kwa kupunguza ulaji wako wa vyakula vilivyochakatwa sana : nyama zenye chumvi nyingi (kama vile chakula cha haraka na nyama iliyokaushwa), chipsi zenye chumvi na vitafunwa vyenye chumvi nyingi (kama vile soda, vitoweo na mikate).

Hivi sasa, hadi 70% ya chumvi katika lishe ya Marekani hutumiwa kutoka kwenye vyakula vilivyosindikwa.

Badala yake, zingatia vyakula ambavyo havijaongezwa sodiamu na sukari na potasiamu na nyuzinyuzi nyingi, kama vile vyakula vya mimea ambavyo havijasindikwa: maharagwe, karanga, mbegu, nafaka, matunda na mboga.

Vyakula vilivyochachushwa, ilhali kwa kawaida huwa na sodiamu nyingi, vinaweza pia kuwa chaguo bora kiafya.

Hatimaye, fikiria uwiano wa sodiamu na potasiamu katika chakula. Ingawa sodiamu husaidia kuweka maji katika mishipa ya damu, potasiamu husaidia kuweka maji katika seli.

Sodiamu ya chakula hutumiwa vyema kwa uwiano wa usawa.

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga.

Karibu AfyaUpdates Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In https://afyaclass.com  Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa4 weeks ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa1 month ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa2 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa2 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa3 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake4 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa1 day ago

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 days ago

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi Madhara ya kula nyama ya ng’ombe mbichi Ni desturi ya baadhi ya watu kula...

Magonjwa1 week ago

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani Mkojo kuuma au kupata maumivu wakati wa kukojoa ni hali ambayo kwa kitaalam...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono dalili Zake

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa2 weeks ago

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu Haya ni maneno ambayo umekuwa ukiyasikia sana linapokuja swala la vipimo cha UKIMWI, je...

Magonjwa3 weeks ago

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia. Kutana na Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa unaosababishwa na konokono

Ugonjwa unaosababishwa na konokono Ugonjwa unaosababishwa na konokono unaitwa schistosomiasis, au bilharzia. Ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na minyoo wanaoitwa...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake. Wengi tumesikia kuhusu Red Eyes(Macho mekundu) Lakini je umewahi kusikia kuhusu Pink Eyes,?...

Magonjwa3 weeks ago

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapa

Omeprazole inatibu ugonjwa gani Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi...

Magonjwa4 weeks ago

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani Mate kujaa Mdomoni,ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na zipo...