Connect with us
Author 1 Author 2 Author 3 Author 4
Authors

afyatips

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa

Doctor Ombeni

Published

on

277 Views
0 Comments

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa Lakini wakati mwingine hupata dalili hii Uzito Kwenye Moyo.

Kwa mtu mwenye uzito mkubwa, presha ya juu, na ameambiwa ana “uzito kwenye moyo”, mara nyingi kauli hiyo inaweza kumaanisha moyo umeanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi au misuli ya moyo, hasa ukuta wa ventrikali ya kushoto, umekuwa mnene (Left Ventricular Hypertrophy—LVH). Presha ya juu isiyodhibitiwa ni sababu kuu ya hali hii.

Vitu vya kufanya na kuzingatia;

Kudhibiti presha kwa umakini:

Pima presha mara kwa mara na andika majibu ya vipimo vyako. #Fahamu pia hapa jinsi ya kupima presha kwa Usahihi

Kama Umepewa dawa za presha, zitumie kwa mpangilio bila kuacha mwenyewe hata kama unajisikia vizuri.

Dawa zinaweza kuhitajika pamoja na mabadiliko ya mtindo wa maisha kulingana na kiwango cha presha pamoja na hali ya moyo kwa mgonjwa.

Kupunguza uzito taratibu:

Uzito mkubwa huongeza mzigo kwenye moyo na huongeza hatari ya presha.

Lengo si kupunguza uzito haraka, bali kupunguza taratibu kupitia chakula bora na shughuli za mwili salama. Hata kupungua kwa kiasi kidogo kunaweza kusaidia udhibiti wa presha.

-Kupunguza matumizi ya chumvi nyingi

Epuka kuongeza chumvi nyingi kwenye chakula.

Punguza vyakula vilivyosindikwa, chipsi, nyama zilizosindikwa, snacks zenye chumvi nyingi na vyakula vya fast food.

Badala yake Kula Mlo wenye mboga za majani, matunda, nafaka zisizokobolewa, kunde, samaki na protini zisizo na mafuta mengi ni bora kwa afya ya moyo.

-Kufanya mazoezi kwa kiwango kinachofaa

Kutembea ni mwanzo mzuri wa mazoezi kwa changamoto hii.

Kama daktari ameruhusu, kuongeza shughuli za mwili taratibu ikiwemo mazoezi mengine kunaweza kusaidia kupunguza uzito na presha.

Kama ana dalili za moyo, Usianze mazoezi makali bila kupimwa kwanza.

Epuka Matumizi ya Kilevyi chochote

–Kuepuka sigara, Epuka kabsa Matumizi ya Sigara

Sigara huongeza mzigo kwenye moyo na mishipa ya damu.

Mtu mwenye presha na tatizo la moyo anashauriwa kuacha kabisa.

–Kuacha pombe

Matumizi ya Pombe kwa kiasi kikubwa Kunaweza kuongeza presha na kuongeza hatari ya matatizo ya moyo.

Kuchunguza sukari na mafuta kwenye damu

Ni vizuri kupima blood glucose/HbA1c, cholesterol, pamoja na kazi ya figo kwa sababu kisukari, cholesterol na ugonjwa wa figo vinaweza kuongeza hatari ya matatizo ya moyo.

Kufanya Vipimo vya Moyo

Kufanya uchunguzi wa moyo Kama “uzito kwenye moyo” umetokana na matatizo ya Moyo ni muhimu pia, Fanya kipimo cha ECG, X-ray au ultrasound, hii ni muhimu kujua hasa tatizo ni nini. Echocardiogram (ECHO) inaweza kuonyesha unene wa misuli ya moyo, ukubwa wa vyumba vya moyo na hali ya valves.

Kulala vizuri na kudhibiti msongo wa mawazo

Lala takribani saa 7–9 za usingizi kwa usiku.

Msongo mkubwa wa mawazo, Kukosa usingizi na uzito mkubwa vinaweza kufanya udhibiti wa presha kuwa mgumu.

Dalili za kwenda hospitali haraka

Usisubiri nyumbani kama unapata maumivu/kubanwa kifuani, kupumua kwa shida sana, kuzimia, udhaifu wa ghafla upande mmoja wa mwili, kuongea kwa shida, au presha ikiwa 180/120 mmHg au zaidi,pamoja na Dalili Zingine.

Hakikisha Unaenda hospital au kukutana na Wataalam wa Afya kwa Changamoto na pia;

Kwa Ushauri Zaidi,Elimu na Tiba tuwasiliane kupitia namba +255758286584.

277 Views
0 Comments

How we reviewed this article:

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

Health Topics Letters

QX
A

Makala za Herufi A (30)

C

Makala za Herufi C (90)

D

Makala za Herufi D (154)

F

Makala za Herufi F (144)

H

Makala za Herufi H (27)

J

Makala za Herufi J (104)

K

Makala za Herufi K (149)

M

Makala za Herufi M (350)

N

Makala za Herufi N (35)

S

Makala za Herufi S (76)

T

Makala za Herufi T (216)

U

Makala za Herufi U (294)

V

Makala za Herufi V (48)

LATEST POSTS

Afya News4 hours ago

Tanzania, Algeria kuanza ushirikiano uzalishaji wa DAWA nchini

TANZANIA, ALGERIA KUANZA USHIRIKIANO UZALISHAJI WA DAWA NCHINI Na Andrea Kadege, WAF–Dar es Salaam Tanzania na Algeria kuanza ushirikiano katika...

EVENTS6 hours ago

Waliofichua namna ubongo unavyofanya kazi watunukiwa tuzo ya Nobel

Daktari bingwa wa magonjwa ya akili na mfumo wa neva kutoka Marekani, Karl Deisseroth, pamoja na wanasayansi kutoka Ujerumani, Peter...

afyatips10 hours ago

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa Lakini wakati mwingine hupata dalili hii Uzito...

magonjwa ya wanaume14 hours ago

Kwanini mwanaume anamwaga mapema

Kwanini Mwanaume Anamwaga Mapema? (Premature Ejaculation) Kumwaga mapema au premature ejaculation (PE) ni hali ambapo mwanaume hufika kileleni na kutoa...

afyatips5 years ago

SABABU ZA MTU KUKONDA

KUKONDA • • • • • • SABABU ZA MTU KUKONDA sababu za mtu kukonda kuweza kuwa za moja kwa...

WHO2 days ago

WHO yatoa Taarifa Mpya kuhusu Kipindupindu, Homa ya Uti wa Mgongo na Tauni Duniani

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti mwenendo mpya wa magonjwa matatu ya bakteria yanayoweza kusababisha milipuko na vifo—kipindupindu (cholera), homa...

magonjwa2 days ago

Magonjwa 5 ya MOYO yanayoweza Kuua haraka

Magonjwa ya moyo na mishipa ni miongoni mwa sababu kubwa za vifo duniani. WHO inaeleza kuwa magonjwa ya moyo na...

FEATURES3 days ago

Rubani Asimulia Jinsi Alivyopambana Baada ya Kuchomwa Kisu na Rubani Mwenza Kwenye Ndege ya Flydubai

Rubani wa ndege ya Flydubai, Captain Smit Machchhar, amesimulia tukio la kutisha lililotokea ndani ya chumba cha marubani baada ya...

Hospital3 days ago

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku, hali inayodhihirisha ukubwa wa tatizo...

Utafiti3 days ago

Maambukizi Yanayozuilika Yasababisha Moja Kati ya Kesi Nane za Saratani Duniani

Utafiti mpya wa Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC), ambalo ni sehemu ya Shirika la Afya Duniani (WHO),...

278
0