Connect with us

magonjwa ya watoto

Mtoto kuharisha baada ya kunyonya chanzo na Tiba yake

Doctor Ombeni

Published

on

Mtoto kuharisha baada ya kunyonya chanzo na Tiba yake

Mtoto kuharisha baada ya kunyonya inaweza kusababishwa na mambo kadhaa, na inategemea umri wake, aina ya maziwa anayonyonya (ya mama au ya kopo), na dalili nyingine anazoonyesha.

Mtoto kuharisha baada ya kunyonya chanzo chake:

1.Mabadiliko ya maziwa ya mama

Maziwa ya mama yana sehemu mbili: “foremilk” (nyepesi yenye sukari) na “hindmilk” (nzito yenye mafuta).

Mtoto akinyonya muda mfupi sana, anapata zaidi foremilk ambayo inaweza kusababisha tumbo kujaa gesi na kuharisha maji.

2.Lishe ya mama anayenyonyesha

Mama akila vyakula vyenye viungo vikali, maziwa, au dawa fulani, vinaweza kuathiri maziwa na kumfanya mtoto apate kuharisha.

3.Maziwa ya kopo (formula milk)

Baadhi ya watoto hawawezi kuvumilia protini fulani kwenye maziwa ya kopo (cow’s milk protein intolerance).

Hii husababisha kuharisha, gesi, na wakati mwingine vipele.

4.Maambukizi ya tumboni (bakteria au virusi)

Vimelea kama rotavirus au E. coli vinaweza kusababisha kuharisha baada ya kunyonya au kula.

5.Kunyonyesha vibaya

Mtoto akimeza hewa nyingi wakati wa kunyonya, au ananyonya kwa nguvu bila kupumzika, tumbo hujaa hewa na kusababisha kuharisha au kutapika.

6.Mzio (allergy) au lactose intolerance

Watoto wachache huwa na lactose intolerance — hawawezi kumeng’enya sukari ya maziwa vizuri, hivyo wanaishia kuharisha baada ya kila unyonyaji.

Dalili za Hatari (Mpeleke Hospitali Haraka) ukiona;

-Kuharisha zaidi ya mara 5 kwa siku.

-Kinyesi chenye damu au rangi ya kijani kibichi sana.

-Mtoto anapoteza maji mwilini,dalili unazoweza kuziona;

  • midomo kuwa mikavu, 
  • macho kudidimia au kuingia ndani zaidi,
  • Mtoto hana machozi anapolia n.k.

-Kukosa hamu ya kunyonya au usingizi mwingi kupita kiasi.

-Homa au kutapika kila mara.

Msaada wa Haraka Nyumbani

Endelea kumnyonyesha mara kwa mara — maziwa ya mama yana maji na kinga.

Usimpe dawa bila ushauri wa daktari.

Ikiwa kuharisha kumezidi sana, anza kumnywesha ORS (maji ya chumvi-sukari) kidogo kidogo mara kwa mara.n.k….

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti9 hours ago

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50 Chanzo: CNN Health Mwandishi: Jacqueline Howard Tarehe: Novemba 12, 2026...

magonjwa ya watoto11 hours ago

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto,fahamu hapa

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto: Sababu, Dalili, Magonjwa Yanayoonekana Mara kwa Mara na Njia za Kuzuia Ngozi ni kiungo kikubwa...

Utafiti16 hours ago

Asilimia 63 ya Wauzaji wa Matunda Wanatumia Kemikali Kuchelewesha au Kuharakisha Kuiva kwa Ndizi na Nyanya

Wataalamu waonya kuhusu matumizi yasiyo sahihi ya kemikali katika kuiva kwa matunda, wakisema baadhi ya kemikali zinaweza kuwa na madhara...

WHO1 day ago

WHO yatoa Miongozo ya Kwanza ya Utambuzi na Udhibiti wa Kisukari cha Aina ya Kwanza kwa Watu Wazima

Shirika la Afya Duniani (World Health Organization – WHO) limetoa kwa mara ya kwanza miongozo ya kimataifa kuhusu utambuzi na...

magonjwa ya wanaume2 years ago

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo Tabia hii imekuwa ikiwaathiri Wanaume Wengi kwa hivi Sasa,Je unazifahamu athari au...

magonjwa1 day ago

HPV ni Ugonjwa gani?,Fahamu hapa

Human Papilloma Virus (HPV): Maana Yake, Magonjwa Inayosababisha Na Athari Zake Kwa Afya Human Papilloma Virus (HPV) ni nini? Human...

Hospital1 day ago

Waziri wa Afya,amewapongeza watumishi wanne kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto

Waziri wa Afya,amewapongeza watumishi wanne kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto Waziri wa Afya, Mohamed Omary Mchengerwa, amewapongeza watumishi...

Ebola2 days ago

Ugonjwa wa Ebola ulivyoleta Athari kwa watoto DRC

Ugonjwa wa Ebola ulivyoleta Athari kwa watoto DRC Kufikia tarehe 4 Novemba, watoto 2,959 wenye umri chini ya miaka 18...

magonjwa ya wanawake3 days ago

Madhara ya kuvurugika kwa homoni za kike (Hormonal Imbalance in women)

Kuvurugika kwa hormone au vichocheo ni nini? Kuvurugika kwa hormone au vichocheo hutokea pale mwili unapozalisha homoni kwa kiwango kikubwa...

Hospital4 days ago

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery)

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery) Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kuboresha huduma za kibingwa...