Kitovu cha Mtoto
Tatizo la KITOVU cha mtoto mchanga hakikauki,Kinatoa Usaha,Damu
Imeboreshwa July 10, 2026 by Doctor Ombeni
KITOVU cha mtoto mchanga hakikauki,Kinatoa Usaha,Damu,Sababu ni nini?
Zipo dalili mbali mbali huweza kujitokeza kwenye Kitovu cha Mtoto wako,Ukiona Dalili hizi,hakikisha Mtoto anapata Msaada, Dalili hizi ni hatarishi sio nzuri wake:
- Kitovu kinatoa usaha wenye harufu mbaya
- Damu inatoka mara kwa mara
- Ngozi kuzunguka kitovu kuwa nyekundu au kuvimba
- Mtoto ana homa au analia sana
- Kitovu hakikauki hata baada ya siku 7–14
Sababu zinazoweza kusababisha
1.Maambukizi ya bakteria (kutokana na uchafu au utunzaji mbaya)
2.Kitovu kubaki na unyevunyevu muda mrefu
3.Kitovu Kuguswa na vitu vichafu (mfano majivu, mafuta, dawa za asili zisizo salama) n.k
Nini cha kufanya
Hii ni hali ya muhimu—usichelewe:
Mpeleke mtoto hospitali au kituo cha afya mara moja Au Ongea na Mtaalam wa Afya au Kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane hapa hapa afyaclass,kupitia namba +255758286584(Call,Sms,Whatsapp).
-Usitumie dawa za kienyeji au kubonyeza kitovu bila Ushauri Sahihi.
-Acha kitovu kiwe kikavu (dry cord care) usiweke maji au Vitu vitakavyoongeza unyevu unyevu
-Epuka kukifunika kwa diaper
-Usikigusie mara kwa mara
Kwa mtoto mchanga, maambukizi ya kitovu yanaweza kuenea haraka mwilini, hivyo ni muhimu kuchukua hatua mapema.
YAPO BAADHI YA MAMBO MUHIMU SANA YA KUZINGATIA KUHUSU KITOVU CHA MTOTO
1-Mama hakikisha kitovu cha mtoto hakivuji damu baada ya kukatwa na kufungwa na mtaalam wa afya.
2-Kitovu hudondoka chenyewe,ambapo kwa asilimia kubwa kwa watoto wengi ndani ya wiki moja,kitovu huwa tayari kimeshadondoka.
3-Hakikisha kitovu cha mtoto hakitoi usaha,au kubalika rangi hasa ya manjano na kutoa harufu mbaya,hii sio dalili nzuri.
4-Usiweke kitu chochote kwenye kitovu cha mtoto mpka kidondoke chenyewe.
5-Epuka imani potofu kama zile za kuweka mavi ya Ng’ombe n.k,kwenye kitovu cha mtoto.
KWA USHAURI,ELIMU AU MSAADA WA KIAFYA MAWASILIANO NI +255758286584.
-
magonjwa2 years ago
Muwasho sehemu za siri kwa mwanaume chanzo chake
-
jinsi ya kupunguza tumbo2 years ago
Mbinu za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka
-
Afya ya mtoto2 years agoMambo ya kuzingatia kwenye utunzaji wa Kitovu cha Mtoto mchanga
-
Madhara ya mtoto kunywa maji machafu4 weeks agoMadhara ya mtoto kunywa maji machafu au maji ya uzazi
-
Madhara ya Pombe3 weeks agoJE, POMBE hupunguza testosterone na Ubora wa mbegu za Kiume?
-
afya5 years agoCHANZO CHA TATIZO LA KUPASUKA MIGUU KWENYE KISIGINO(gaga)
-
uzazi1 week agoVyakula vya kuongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha
-
afya5 years agoFAHAMU KUHUSU VIRUSI VYA CORONA NA UGONJWA WA COVID 19(chanzo,dalili,madhara,tiba)




