Connect with us

magonjwa ya watoto

Mtoto kujisaidia kinyesi cha kamasi

Doctor Ombeni

Published

on

Imeboreshwa July 25, 2026 by Doctor Ombeni

Mtoto Kujisaidia Kinyesi Chenye Kamasi: Je, Ni Kawaida au Ni Dalili ya Tatizo?

Wazazi wengi hushtuka wanapoona mtoto amejisaidia kinyesi chenye kamasi (uteute unaofanana na makamasi). Hali hii ikiwa ya mara kwa mara au Ikiambatana na damu, homa au maumivu makali inaweza kuashiria tatizo linalohitaji uchunguzi wa daktari.

Kamasi kwenye kinyesi husababishwa na nini?

Sababu zinazoweza kusababisha hali hii ya kijisaidia kinyesi chenye makamasi kwa watoto ni pamoja na:

  • Maambukizi ya utumbo yanayosababishwa na virusi, bakteria au vimelea vya magonjwa kama Amiba.
  • Mzio wa protini ya maziwa ya ng’ombe (Cow’s Milk Protein Allergy – CMPA) hasa kwa watoto wachanga.
  • Kuharisha (gastroenteritis) ambapo kamasi huambatana na choo cha maji.
  • Kuvimbiwa kwa muda mrefu (constipation) ambako kunaweza kusababisha ute kutoka kwenye utumbo.
  • Magonjwa ya uchochezi wa utumbo, ingawa ni nadra kwa watoto wadogo.

Ukiona Dalili hizi, mtoto anahitaji Msaada wa haraka

Hakikisha Mtoto anapata Msaada wa tiba haraka ikiwa unaona:

  • Damu kwenye kinyesi chake
  • Kamasi nyingi zinazoendelea kwa siku kadhaa.
  • Homa kali.
  • Kuharisha sana au kutapika na dalili za upungufu wa maji mwilini.
  • Maumivu makali ya tumbo.
  • Kushindwa kula au kunywa vizuri.
  • Kupungua uzito au kuonekana dhaifu.

Wazazi wana uzoefu gani?

Wazazi wengi huripoti kuwa walipoona kamasi kwenye kinyesi walidhani ni kuhara kwa kawaida. Baadhi ya watoto walipopimwa waligundulika kuwa na maambukizi ya utumbo, huku wengine wakibainika kuwa na mzio wa maziwa ya ng’ombe. Wazazi wengi wanasisitiza kuwa kutafuta ushauri wa daktari mapema kulisaidia kubaini chanzo na kuanza matibabu sahihi mapema.

Madaktari wanasemaje?

Madaktari wa Afyaclass,Mayo clinic,Healthline n.k, wanaeleza kuwa,ukiona kamasi nyingi au hali hii kujirudia mara kwa mara, hasa ikifuatana na damu, kuharisha au maumivu ya tumbo, inahitaji uchunguzi wa daktari ili kubaini chanzo na kutoa matibabu sahihi.

Takwimu

  • Magonjwa ya kuhara bado ni miongoni mwa sababu kuu za watoto kupata matibabu duniani, na maambukizi ya utumbo ni moja ya sababu zinazoweza kusababisha kinyesi chenye kamasi.

Kumbuka;

Ikiwa kamasi ni nyingi, zinajirudia, zinaambatana na damu, homa, maumivu makali au mtoto anaonekana kudhoofika, hakikisha mtoto wako anapata msaada haraka kutoka kwa wataalam wa afya au;

Kwa Ushauri zaidi na Tiba tuwasiliane hapa hapa ndani ya afyaclass kwa namba +255758286584.

References;

  • https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/inflammatory-bowel-disease/expert-answers/mucus-in-stool/faq-20058262
  • https://www.nhs.uk/conditions/dysentery/
  • https://www.nhs.uk/symptoms/bleeding-from-the-bottom-rectal-bleeding/
  • https://www.nhs.uk/symptoms/soiling-child-pooing-their-pants/

🏆Certified| Doctor from Afyaclass.Hapa utapata Ushauri & Tiba juu ya magonjwa mbali mbali. Kwa msaada Zaidi Tuwasiliane kupitia namba: +255758286584.Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *