Connect with us

afyatips

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA TRIKOMONASI,CHANZO,DALILI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Doctor Ombeni

Published

on

 TRIKOMONASI

• • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA TRIKOMONASI,CHANZO,DALILI PAMOJA NA MATIBABU YAKE


Trikomonasi ni miongoni mwa magonjwa ya zinaa, Tatizo hili mtu huweza kulipata kwa njia ya kujamiiana.


CHANZO CHA TATIZO HILI LA TRIKOMONASI


Ugonjwa huu wa Trikomonasi hutokana na mtu kupata maambukizi ya vimelea aina ya PROTOZOA vinavyojulikana kwa jina la TRICHOMONAS VAGINALIS.


DALILI ZA UGONJWA WA TRIKOMONASI NI PAMOJA NA;


(a) Kwa Wanawake


1. Mgonjwa kupata miwasho sehemu za siri ambapo hupata miwasho maeneo ya kuzunguka ukeni ikiwemo pamoja na ngozi ya mashavu ya uke.


2. Kutokwa na uchafu sehemu za siri  wenye rangi kama njano,nyeupe au Kijani kwa mwanamke


3. Mwanamke kuvuja damu sehemu za siri


4. Ngozi ya sehemu za siri kubadilika rangi na kuwa nyekundu pamoja na kuvimba


5. Kuhisi hali kama ya kuungua sehemu za siri mara kwa mara


6. Kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa


7.Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa


8. Kupata hisia za mkojo mara kwa mara ndani ya mda mfupi


(b). Kwa Wanaume


1. Mgonjwa kupata miwasho sana sehemu za siri, kwenye Njia ya Mkojo ikiwemo eneo la kitundu kidogo cha mkojo kwenye uume


2. Kutokwa na uchafu kwenye Njia ya mkojo


3. Kuhisi hali ya kuchomwa au kuungua baada ya mwanaume kutoa mbegu za kiume au baada ya mwanaume kumwaga shahawa akifanya mapenzi


4. Kuhisi hali ya kuungua au kuchomwa wakati wa kukojoa


5. Kupata hisia za kukojoa mara kwa mara ndani ya mda mfupi


WATU AMBAO WAPO KATIKA HATARI YAKUPATA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;


1. Watu wenye wapenzi wengi


2. Watu ambao wameshawahi kupata tatizo hili hapo nyuma


3. Watu ambao wanashiriki mapenzi bila kinga au wanaofanya ngono zembe


4. Watu wenye historia ya kupata magonjwa mengine ya zinaa kama kaswende au kisonono


MATIBABU YA UGONJWA HUU WA TRIKOMONASI


Ugonjwa huu hutibika na moja ya matibabu makubwa ni pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali jamii ya Antibiotics. Mgonjwa huweza kupewa dawa aina ya Tinidazole pamoja na Metronidazole hilo tatizo likaisha kabsa.

–

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.







✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

magonjwa ya Zinaa2 weeks ago

Ugonjwa wa Genital herpes,chanzo,dalili na Tiba

HERPES SEHEMU ZA SIRI: DALILI, NAMNA INAVYOAMBUKIZWA, KINGA NA MATIBABU Herpes sehemu za siri (Genital herpes) ni maambukizi ya zinaa...

magonjwa1 day ago

Ugonjwa wa Hepatitis C,chanzo chake,Dalili na Tiba

Ugonjwa wa Hepatitis C,chanzo chake,Dalili na Tiba Hepatitis C ni nini? Hepatitis C ni ugonjwa unaosababisha kuvimba na kuharibika kwa...

Uzazi&Ujauzito2 years ago

Dalili za mimba changa kuanzia wiki mbili hadi miezi mitatu ya ujauzito

Dalili za mimba changa kuanzia wiki mbili hadi miezi mitatu ya ujauzito. Fahamu Dalili za mimba changa kuanzia wiki mbili...

Ebola1 day ago

Baada ya kuthibitishwa kwa wagonjwa tisa nchini Kenya

Baada ya kuthibitishwa kwa wagonjwa tisa nchini Kenya Takriban wafanyakazi 5,000 wa sekta ya afya wamepewa mafunzo ya jinsi ya...

Ebola1 day ago

Hakuna haja ya hofu: Serikali ya Nigeria yasema baada ya mwanamke kupatikana na Ebola katika eneo la FCT

Hakuna haja ya hofu: Serikali ya Nigeria yasema baada ya mwanamke kupatikana na Ebola katika eneo la FCT Oktoba 20,...

Ebola1 day ago

Nigeria imethibitisha kisa cha Ebola katika mji mkuu Abuja

Nigeria imethibitisha kisa cha Ebola katika mji mkuu Abuja, baada ya mwanamke aliyewasili kutoka Uganda kukutwa na virusi vya ugonjwa...

Ukimwi2 days ago

Maambukizi ya virusi vya ukimwi

Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (Vvu): Njia Za Maambukizi Na Namna Ya Kujikinga Virusi vya UKIMWI (VVU) ni nini? Virusi...

magonjwa2 days ago

Maambukizi ya bakteria wa shigella: dalili, njia za maambukizi, Matibabu Na Kinga

Shigella ni aina ya bakteria wanaosababisha ugonjwa unaojulikana kama shigellosis, ambao huathiri mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, hasa utumbo mpana....

magonjwa ya wanaume4 days ago

Mwanaume kushindwa kutungisha mimba

Tumezoea kwenye jamii Zetu Mara nyingi linapokuja Swala la kutokupata Mtoto,Lawama zote ni kwa Mwanamke,Lakini fahamu hata mwanaume anaweza kuwa...

Stars Health3 days ago

Papa aanza kurejea taratibu katika majukumu yake baada ya upasuaji wa Saratani ya Mapafu

Vatican, Oktoba 18, 2026 — Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Papa Leo, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani mwenye umri wa...