Connect with us
Author 1 Author 2 Author 3 Author 4
Authors

magonjwa

Ugonjwa Wa Guillain-barre Syndrome,Chanzo,Dalili Na Tiba Yake

Doctor Ombeni

Published

on

114 Views
0 Comments

 UGONJWA WA GUILLAIN-BARRE SYNDROME,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE

Guillain-Barre syndrome huu ni ugonjwa ambao hutokea mara chache sana na ugonjwa huu huhusisha Mfumo wa kinga ya mwili yaani Body immunity system kushambulia mfumo wa fahamu au Nerves zako mwilini.

DALILI ZA UGONJWA WA GUILLAIN-BARRE SYNDROME

Ugonjwa huu huhusisha dalili pamoja na Ishara mbali mbali ikiwa ni pamoja na;

1. Misuli ya mwili kuanza kudhoofika na kukosa nguvu kabsa,na udhaifu huu huanzia kwenye misuli ya miguuni kisha kusambaa kwenye maeneo mbali mbali ya mwili kama Mikononi n.k

2. Mtu kuhisi hali ya kuchomwa na kitu cha ncha kali kama sindano kwenye vidole vya miguuni,mikononi,kwenye kisigino cha mguuni n.k

3. Mtu kutembea kwa  shida,kushindwa kutembea kabsa au kushindwa kupanda ngazi sehemu ambapo kuna ngazi

4. Mtu kupata shida ya kuongea,kushindwa kutafuna au kumeza kitu chochote

5. Mtu kupata shida ya kuona au kuona marue rue yaani double vision

6. Kupata maumivu makali ya viungo mbali mbali vya mwili hasa wakati wa usiku

7. Mtu Kushindwa kudhibiti utendaji kazi wa kibofu chake cha mkojo, hali ambayo huweza kusababisha matatizo kama kujikojolea n.k

8. Mtu kupata tatizo la Mapigo ya moyo kwenda mbio

9. Mtu Kuwa na tatizo la Presha kushuka au kupanda

10. Mtu kupata shida sana wakati wa upumuaji n.k

CHANZO CHA TATIZO HILI LA GUILLAIN-BARRE SYNDROME

Mpaka sasa chanzo cha moja kwa moja dhidi ya ugonjwa huu hakijajulikana, ila kuna baadhi ya sababu ambazo zimeonekana kuongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili na sababu hizo ni kama vile;

– Kuwa na umri mkubwa lakini pia tafiti zinaonyesha ugonjwa huu hushambulia wanaume zaidi ya wanawake

– Mtu kushambuliwa na bacteria anayejulikana kwa jina la campylobacter,bacteria huyu hupatikana kwenye nyama ya kuku ambayo haijaiva vizuri

– Mtu kushambuliwa na virusi mbali mbali kama vile; Virusi vya mafua yaani Influenza virus,Cytomegalovirus,Epstein-Barr virus,Zika virus n.k

– Mashambulizi ya homa ya Ini Kama vile HEPATITIS A,B,C na E

– Maambukizi ya virusi vya ukimwi yaani HIV/AIDS

– Mtu kupatwa na ugonjwa wa Pneumonia kama vile Mycoplasma pneumonia n.k

– Mtu kufanyiwa upasuaji wa aina mbali mbali mwilini

– Mtu kupata ajali au kuumia pamoja na kupatwa na matatizo mengine kama vile Hodgkin’s lymphoma n.k

MADHARA YA TATIZO HILI LA GUILLAIN-BARRE SYNDROME

kama nilivyokwisha kuelezea hapo mwanzo kwamba tatizo hili huhusisha mfumo wa kinga ya mwili kushambulia NERVES zako mwilini,hivo moja kwa moja mgonjwa hupata madhara yanayotokana na uharibifu wa Nerves mwilini kama vile;

• Kupumua kwa shida au kupata shida ya upumuaji

• Misuli ya mwili kuwa dhoofu hasa miguuni na kupelekea mtu kushindwa kutembea n.k

• Mtu kuhisi hali ya kuchomwa na kitu cha ncha kali kama sindano kwenye vidole vya miguuni,mikononi,kwenye visigino n.k

• Mtu kuanza kuwa na matatizo ya Presha au shinikizo la damu

• Mtu kuanza kuwa na matatizo mbali mbali ya moyo

• Mtu kuhisi maumivu makali ya viungo

• Mtu kushindwa kudhibiti utokaji wa mkojo

• Mtu kuanza kupata tatizo la damu kuganda au kutengeneza clots,kuwa na vidonda yaani Pressure sores hii ni kutokana na mtu kulala kwa muda mrefu au kutokuwa na uwezo wa kutembea mara kwa mara

MATIBABU YA TATIZO HILI LA GUILLAIN-BARRE SYNDROME

Hakuna tiba ya kuondoa kabsa tatizo hili,ila kuna matibabu ya kudhibiti dalili zinazotokana na tatizo hili na kumsaidia mgonjwa kurecover kama mwanzoni ingawa bado tatizo analo mwilini mwake, na matibabu hayo ni kama vile;

✓ Tiba ya Plasma exchange yaani plasmapheresis

✓Huduma ya Immunoglobulin therapy, ambapo mgonjwa hupewa Immunoglobulin ambazo zina Antibodies salama yaani healthy antibodies kutoka kwa mtu aliyemchangia damu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

114 Views
0 Comments

How we reviewed this article:

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

Health Topics Letters

QX
A

Makala za Herufi A (30)

C

Makala za Herufi C (90)

D

Makala za Herufi D (154)

F

Makala za Herufi F (144)

H

Makala za Herufi H (27)

J

Makala za Herufi J (104)

K

Makala za Herufi K (149)

M

Makala za Herufi M (350)

N

Makala za Herufi N (35)

S

Makala za Herufi S (76)

T

Makala za Herufi T (216)

U

Makala za Herufi U (294)

V

Makala za Herufi V (48)

LATEST POSTS

Afya News7 hours ago

Tanzania, Algeria kuanza ushirikiano uzalishaji wa DAWA nchini

TANZANIA, ALGERIA KUANZA USHIRIKIANO UZALISHAJI WA DAWA NCHINI Na Andrea Kadege, WAF–Dar es Salaam Tanzania na Algeria kuanza ushirikiano katika...

EVENTS9 hours ago

Waliofichua namna ubongo unavyofanya kazi watunukiwa tuzo ya Nobel

Daktari bingwa wa magonjwa ya akili na mfumo wa neva kutoka Marekani, Karl Deisseroth, pamoja na wanasayansi kutoka Ujerumani, Peter...

afyatips12 hours ago

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa Lakini wakati mwingine hupata dalili hii Uzito...

magonjwa ya wanaume16 hours ago

Kwanini mwanaume anamwaga mapema

Kwanini Mwanaume Anamwaga Mapema? (Premature Ejaculation) Kumwaga mapema au premature ejaculation (PE) ni hali ambapo mwanaume hufika kileleni na kutoa...

afyatips5 years ago

SABABU ZA MTU KUKONDA

KUKONDA • • • • • • SABABU ZA MTU KUKONDA sababu za mtu kukonda kuweza kuwa za moja kwa...

WHO2 days ago

WHO yatoa Taarifa Mpya kuhusu Kipindupindu, Homa ya Uti wa Mgongo na Tauni Duniani

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti mwenendo mpya wa magonjwa matatu ya bakteria yanayoweza kusababisha milipuko na vifo—kipindupindu (cholera), homa...

magonjwa2 days ago

Magonjwa 5 ya MOYO yanayoweza Kuua haraka

Magonjwa ya moyo na mishipa ni miongoni mwa sababu kubwa za vifo duniani. WHO inaeleza kuwa magonjwa ya moyo na...

FEATURES3 days ago

Rubani Asimulia Jinsi Alivyopambana Baada ya Kuchomwa Kisu na Rubani Mwenza Kwenye Ndege ya Flydubai

Rubani wa ndege ya Flydubai, Captain Smit Machchhar, amesimulia tukio la kutisha lililotokea ndani ya chumba cha marubani baada ya...

Hospital3 days ago

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku, hali inayodhihirisha ukubwa wa tatizo...

Utafiti4 days ago

Maambukizi Yanayozuilika Yasababisha Moja Kati ya Kesi Nane za Saratani Duniani

Utafiti mpya wa Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC), ambalo ni sehemu ya Shirika la Afya Duniani (WHO),...

115
0