magonjwa
UTUMBO KUJIKUNJA(UTUMBO MKUBWA & UTUMBO MDOGO),VISABABISHI VYAKE PAMOJA NA DALILI ZAKE
Utumbo Kujikunja(Utumbo Mkubwa & Utumbo Mdogo),Visababishi Vyake Pamoja Na Dalili Zake
Tatizo la Utumbo kujikunja huweza kutokea kwa mtu wa Umri wowote, ambapo kwa mtu mzima utumbo kujikunja kitaalam huitwa VOLVULUS na kwa watoto wadogo ambapo utumbo huingia ndani hujulikana kama INTUSUSSEPTION.
(Intestinal volvulus) ni hali ambapo utumbo hujizungusha wenyewe na kusababisha kuziba kwa njia ya chakula na wakati mwingine kukata mzunguko wa damu kwenye sehemu ya utumbo. Ikiwa haitatibiwa haraka, inaweza kuwa hatari kwa maisha hata kusababisha Kifo.
ZIPO SABABU MBALI MBALI AMBAZO HUWEZA KUCHANGIA KUTOKEA KWA TATIZO HILI
Sababu hizo ni pamoja na;
✓ Mtu kupata choo kigumu kwa mda mrefu( hali ya kudumu) au Kwa kitaalam huitwa Chronic Constipation
✓ Kupatwa na minyoo ya Utumbo maarufu kama Round worms
✓ Kukaa Mda mrefu bila kula Chakula
✓ Kuwahi kufanyiwa operation ya utumbo hapo nyuma
✓ Matumizi ya Laxatives kwa wingi
✓ Umri pia huweza kuchangia kuwepo kwa shida hii
Dalili zinazoweza kuonekana
- Maumivu makali ya tumbo yanayoanza ghafla.
- Tumbo kuvimba.
- Kutapika.
- Tumbo kujaa gesi au Kukosa choo.
- Homa (ikiwa maambukizi yameanza).
DALILI ZA UTUMBO KUJIKUNJA
Dalili za Utumbo Kujikunja ni pamoja na;
-Mgonjwa kuvimba tumbo upande mmoja
– Tumbo kujaaa
– Hali ya kukosa choo
– Kupatwa na homa
– Mapimo ya moyo kwenda mbio
– Maumivu makali sana ya tumbo hasa ukijaribu kulishika
Kwa ushauri zaidi, elimu au Tiba Tuwasiliane Kwa Namba +255758286584.
Madhara ya Utumbo Kujikunja
Madhara ya utumbo kujikunja ni pamoja na;
- Kuziba kwa utumbo – Chakula, gesi na kinyesi hushindwa kupita kwa Sababu ya utumbo kuziba.
- Kukatika kwa mzunguko wa damu – Sehemu ya utumbo hukosa damu na kuanza kufa (intestinal ischemia).
- Utumbo kupasuka (Perforation) – Ukuta wa utumbo unaweza kupasuka au kutoboka na kuruhusu uchafu kuingia tumboni.
- Maambukizi makali ya tumbo (Peritonitis) – Hali hii ni dharura ya kitabibu na inaweza kuhatarisha maisha.
- Mshtuko wa mwili (Septic shock) – Maambukizi makali yanaweza kusababisha kushuka kwa shinikizo la damu na kushindwa kwa viungo muhimu mwilini.
- Kifo – Endapo matibabu hayatapatikana kwa wakati kifo huweza kutokea kwa mgonjwa husika.
Hii ni hali ya dharura inayohitaji mgonjwa apelekwe hospitali mara moja kwa uchunguzi na matibabu ya haraka, ambayo mara nyingi huweza kuhusisha upasuaji.
References (APA 7th Edition);
- Merck Manual Professional Edition. (2025). Intestinal obstruction. https://www.merckmanuals.com/professional/gastrointestinal-disorders/acute-abdomen-and-surgical-gastroenterology/intestinal-obstruction
- National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. (2023). Intestinal obstruction. https://www.niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/intestinal-obstruction
- World Health Organization. (2023). Integrated management for emergency and essential surgical care. https://www.who.int
- Jameson, J. L., Fauci, A. S., Kasper, D. L., Hauser, S. L., Longo, D. L., & Loscalzo, J. (Eds.). (2022). Harrison’s principles of internal medicine (21st ed.). McGraw Hill.
- Brunicardi, F. C., Andersen, D. K., Billiar, T. R., Dunn, D. L., Kao, L. S., Hunter, J. G., & Matthews, J. B. (2022). Schwartz’s principles of surgery (12th ed.). McGraw Hill.
In-text citation:
- (Merck Manual Professional Edition, 2025)
- (National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases [NIDDK], 2023)
- (Jameson et al., 2022)
- (Brunicardi et al., 2022
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa








Jackson Mathiasi
September 5, 2026 at 6:15 am
Naelewa sasa,Mtaalam,umeeleza vizuri jambo hili
Doctor Ombeni
September 5, 2026 at 6:16 am
Asante sana