Connect with us
Author 1 Author 2 Author 3 Author 4
Authors

afyatips

JE KWANINI NI MUHIMU KUZINGATIA ULAJI MZURI?

Doctor Ombeni

Published

on

101 Views
0 Comments

ULAJI

• • • • • •

JE KWANINI NI MUHIMU KUZINGATIA ULAJI MZURI?


Ulaji unaofaa ni pamoja na kula chakula mchanganyiko, cha kutosha na chenye virutubishi vyote kwa uwiano unaotakiwa. Kula matunda angalau mara mbili kwa siku na kula mboga mboga kwa wingi.

Ulaji unaofaa ni lazima uzingatie matumizi ya mafuta kwa kiasi kidogo. Mafuta ya nyama sio mazuri sana kwani yanahusishwa na magonjwa ya moyo, badala yake inashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokanayo na mimea. 

Kama vile mafuta ya alizeti n.k

Matumizi ya sukari na chumvi yawe ya kiasi. Pia kwa watu wanaokunywa pombe wasinywe kupita kiasi.


KULA CHAKULA MCHANGANYIKO

Chakula mchanganyiko hukuwezesha kupata virutubishi vyote vinavyohitajika mwilini, kwa mfano vyakula vya wanga vinasaidia kuupa mwili nguvu na joto, utomwili husaidia kujenga mwili, vitamini na madini hulinda mwili dhidi ya magonjwa. Kila siku jitahidi kula vyakula kutoka katika makundi yafuatatyo: Vyakula vya asili ya nafaka, ndizi za kupika na mizizi

Vyakula vya jamii ya kunde, asili ya wanyama na mbegu za mafuta

Mboga mboga

Matunda

Sukari, asali na mafuta


KUTOKULA MAFUTA MENGI

Mafuta mengi mwilini hasa yale yenye asili ya wanyama yanaweza kusababisha ongezeko la magonjwa ya moyo na shinikizo kubwa la damu, hivyo inashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokanayo na mimea.  JINSI YA KUPUNGUZA MAFUTA:

Tumia mafuta kidogo wakati wa kupika

Epuka kula vyakula vilivyokaangwa kwa mafuta badala yake chemsha, oka au choma

Punguza mafuta kwenye nyama iliyonona, na ikibidi ondoa ngozi ya kuku kabla ya kupika.

Chagua nyama au samaki wasio na mafuta mengi.

Kula matunda na mbogamboga kwa wingi

Vyakula hivi huupatia mwili kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali kama vile baadhi ya magonjwa ya moyo, saratani na kisukari.


MATUNDA NI CHANZO CHA VIRUTUBISHO/VIINILISHE VYA VITAMINI NA MADINI 

ambavyo hupatikana kwa wingi kwenye vyakula hivi kuliko kwenye vyakula vingine. Virutubisho hivi: huifanya ngozi kuwa ng’aavu na yenye afya na vidonda kupona vizuri

huwezesha macho kuona vizuri

husaidia kuimarisha ufahamu

husaidia uyeyushaji wa vyakula tumboni na kufyonza madini mwilini

hutumika katika kutengeneza damu

husaidia katika uundaji wa chembe za uzazi.



101 Views
0 Comments

How we reviewed this article:

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

Health Topics Letters

QX
A

Makala za Herufi A (30)

C

Makala za Herufi C (90)

D

Makala za Herufi D (154)

F

Makala za Herufi F (144)

H

Makala za Herufi H (27)

J

Makala za Herufi J (104)

K

Makala za Herufi K (149)

M

Makala za Herufi M (350)

N

Makala za Herufi N (35)

S

Makala za Herufi S (76)

T

Makala za Herufi T (216)

U

Makala za Herufi U (294)

V

Makala za Herufi V (48)

LATEST POSTS

Afya News5 hours ago

Tanzania, Algeria kuanza ushirikiano uzalishaji wa DAWA nchini

TANZANIA, ALGERIA KUANZA USHIRIKIANO UZALISHAJI WA DAWA NCHINI Na Andrea Kadege, WAF–Dar es Salaam Tanzania na Algeria kuanza ushirikiano katika...

EVENTS7 hours ago

Waliofichua namna ubongo unavyofanya kazi watunukiwa tuzo ya Nobel

Daktari bingwa wa magonjwa ya akili na mfumo wa neva kutoka Marekani, Karl Deisseroth, pamoja na wanasayansi kutoka Ujerumani, Peter...

afyatips11 hours ago

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa Lakini wakati mwingine hupata dalili hii Uzito...

magonjwa ya wanaume15 hours ago

Kwanini mwanaume anamwaga mapema

Kwanini Mwanaume Anamwaga Mapema? (Premature Ejaculation) Kumwaga mapema au premature ejaculation (PE) ni hali ambapo mwanaume hufika kileleni na kutoa...

afyatips5 years ago

SABABU ZA MTU KUKONDA

KUKONDA • • • • • • SABABU ZA MTU KUKONDA sababu za mtu kukonda kuweza kuwa za moja kwa...

WHO2 days ago

WHO yatoa Taarifa Mpya kuhusu Kipindupindu, Homa ya Uti wa Mgongo na Tauni Duniani

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti mwenendo mpya wa magonjwa matatu ya bakteria yanayoweza kusababisha milipuko na vifo—kipindupindu (cholera), homa...

magonjwa2 days ago

Magonjwa 5 ya MOYO yanayoweza Kuua haraka

Magonjwa ya moyo na mishipa ni miongoni mwa sababu kubwa za vifo duniani. WHO inaeleza kuwa magonjwa ya moyo na...

FEATURES3 days ago

Rubani Asimulia Jinsi Alivyopambana Baada ya Kuchomwa Kisu na Rubani Mwenza Kwenye Ndege ya Flydubai

Rubani wa ndege ya Flydubai, Captain Smit Machchhar, amesimulia tukio la kutisha lililotokea ndani ya chumba cha marubani baada ya...

Hospital3 days ago

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku, hali inayodhihirisha ukubwa wa tatizo...

Utafiti3 days ago

Maambukizi Yanayozuilika Yasababisha Moja Kati ya Kesi Nane za Saratani Duniani

Utafiti mpya wa Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC), ambalo ni sehemu ya Shirika la Afya Duniani (WHO),...

102
0