Connect with us
Author 1 Author 2 Author 3 Author 4
Authors

afyatips

UGONJWA WA FISTULA MAANA YAKE,CHANZO CHAKE,DALILI NA TIBA YAKE

Doctor Ombeni

Published

on

165 Views
0 Comments

UGONJWA WA FISTULA KWA WANAWAKE MAANA YAKE,CHANZO CHAKE,DALILI NA TIBA YAKE


Karibu katika makala hii,kujua Zaidi Ugonjwa huu wa FISTULA,Vipo vipengele ambavyo tutavigusia kama ifuatavyo;
  1. Utangulizi Kujua maana ya Ugonjwa wa FISTULA na Aina za Fistula
  2. Chanzo cha Ugonjwa huu wa Fistula
  3. Makundi ambao yapo katika hatari za kupata Ugonjwa wa Fistula
  4. Dalili zote za Ugonjwa wa Fistula
  5. Tiba za Ugonjwa wa Fistula
  6. Maelekezo Jinsi ya kupata Ushauri,Elimu au Tiba kama Unahitaji

🔻SOMO KAMILI

Ugonjwa wa Fistula kwa Wanawake ni nini?

FISTULA kwa Wanawake- Huu ni Ugonjwa unawapata WANAWAKE ambapo unahusisha kuwepo kwa tundu au upenyo katika layer mbili Mfano; Tundu kati ya Njia ya Mkojo na Kibofu cha Mkojo, Tundu kati ya Njia ya Mkojo na Njia ya Haya Kubwa,Tundu kati ya Njia ya Mkojo na Utumbo Mkubwa n.k. Ambapo matokeo yake husababisha mwanamke kushindwa Kujizuia kukojoa, au Uchafu wa Haja Kubwa kutokea Njia ya Haja Ndogo n.k

👉 BAADHI YA AINA ZA UGONJWA WA FISTULA

(1) RectoVaginal Fistula(RVF)- Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya Njia ya Haja Kubwa na Uke wa mwanamke

(2) ColoVaginal Fistula(CVF)-Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya utumbo mkubwa na Uke wa mwanamke

(3) VesicoVaginal Fistula (VVF)- Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya kibofu cha Mkojo na Uke au Njia ya Mkojo ya mwanamke

Chanzo cha Ugonjwa Huu wa FISTULA

  • Majeraha au Tundu ambalo hutokea wakati Mwanamke anajifungua,ambapo linaweza kusabibishwa na uzembe wakati wa upasuaji,au mgandamizo wa mtoto wakati anatoka,au wakati mama anasaidiwa kutolewa mtoto wakati anajifungua kwa Njia ya kawaida,ambapo hii huhusisha matumizi ya vifaa vyenye ncha kali Mfano wakati wa procedure inaitwa Episiotomy au Forceps Delivery.
  • Maambukizi ya Magonjwa mbali mbali kama HIV na magonjwa mengine ya Zinaa,uwepo wa Ugonjwa wa CANCER,Ugonjwa wa TB, na Magonjwa katika Utumbo ambapo kitaalam tunasema Intestinal diseases like;Crohn’s disease and diverticulitis.
  • Matibabu yanayohusisha Mionzi ambapo kitaalam Hujulikana kama RADIATION TREATMENT

Dalili za Ugonjwa wa Fistula

✓ Mwanamke kutokwa na Mkojo pasipo Kujizuia (Dalili kubwa na kiashiria kikubwa cha Ugonjwa wa Fistula)

✓ Uchafu wa Haja Kubwa(Kinyesi) kutoka katika Njia ya Haja Ndogo(ukeni)

✓ Mwanamke kuwa na Harufu ya Mkojo mda wote (Urine Smell)

✓ Mwanamke kutembea kama Amepinda

✓ Mwanamke kunuka Harufu ya Kinyesi

✓ Mwanamke kupata homa,maumivu makali ya Ubavu na Tumbo chini ya kitovu

📶 Kundi Ambalo lipo kwenye Hatari ya Kupata Ugonjwa wa Fistula

– Kuwa mwanamke au Jinsia ya Kike
– Mwanamke Mjamzito na anayejifungua
– Mwanamke mwenye magonjwa kama HIV na magonjwa mengine ya Zinaa(sexual Transmitted Diseases),CANCER,tuberculosis(TB), Magonjwa ya Utumbo ambapo kitaalam tunasema Intestinal diseases like;Crohn’s disease and diverticulitis
– Mwanamke anayepata huduma au tiba ya mionzi- RADIATION TREATMENT

Vipimo; Vipo vipimo mbali mbali,kama vile vya magonjwa yote ya maambukizi,vipimo vya Mkojo,Na pia kufwatilia kwa Makini kuhusu Dalili za Ugonjwa wa Fistula kwa Mgonjwa

TIBA AU MATIBABU YA UGONJWA WA FISTULA

Ugonjwa wa Fistula,baada ya kugundulika zipo njia mbali mbali za Kutibu tatizo hili kulingana na Chanzo cha Tatizo hili,Na Njia hizo ni kama;
👉Mwanamke kufanyiwa Upasuaji kisha kuzibwa sehemu ya Tundu la FISTULA,
👉 Baada ya Upasuaji,mwanamke atapewa dawa mbali mbali ikiwemo za kuzuia na kutibu maambukizi mbali mbali

KUMBUKA; 

Ugonjwa huu wa FISTULA unatibika kabsa,kwahyo basi kama unatatizo hili umekata tamaa,Tiba ipo usiabike,nenda Hosptal kapate matibabu, fistula inatibika kabsa.
#FISTULA #TIBA #USHINDI

@Kwa Ushauri Zaidi,Elimu au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584,Tuma Ujumbe au Piga simu utasikilizwa na kuhudumiwa kwa haraka popote Ulipo.

165 Views
0 Comments

How we reviewed this article:

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

Health Topics Letters

QX
A

Makala za Herufi A (30)

C

Makala za Herufi C (90)

D

Makala za Herufi D (154)

F

Makala za Herufi F (144)

H

Makala za Herufi H (27)

J

Makala za Herufi J (104)

K

Makala za Herufi K (149)

M

Makala za Herufi M (350)

N

Makala za Herufi N (35)

S

Makala za Herufi S (76)

T

Makala za Herufi T (216)

U

Makala za Herufi U (294)

V

Makala za Herufi V (48)

LATEST POSTS

Afya News5 hours ago

Tanzania, Algeria kuanza ushirikiano uzalishaji wa DAWA nchini

TANZANIA, ALGERIA KUANZA USHIRIKIANO UZALISHAJI WA DAWA NCHINI Na Andrea Kadege, WAF–Dar es Salaam Tanzania na Algeria kuanza ushirikiano katika...

EVENTS7 hours ago

Waliofichua namna ubongo unavyofanya kazi watunukiwa tuzo ya Nobel

Daktari bingwa wa magonjwa ya akili na mfumo wa neva kutoka Marekani, Karl Deisseroth, pamoja na wanasayansi kutoka Ujerumani, Peter...

afyatips11 hours ago

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa Lakini wakati mwingine hupata dalili hii Uzito...

magonjwa ya wanaume15 hours ago

Kwanini mwanaume anamwaga mapema

Kwanini Mwanaume Anamwaga Mapema? (Premature Ejaculation) Kumwaga mapema au premature ejaculation (PE) ni hali ambapo mwanaume hufika kileleni na kutoa...

afyatips5 years ago

SABABU ZA MTU KUKONDA

KUKONDA • • • • • • SABABU ZA MTU KUKONDA sababu za mtu kukonda kuweza kuwa za moja kwa...

WHO2 days ago

WHO yatoa Taarifa Mpya kuhusu Kipindupindu, Homa ya Uti wa Mgongo na Tauni Duniani

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti mwenendo mpya wa magonjwa matatu ya bakteria yanayoweza kusababisha milipuko na vifo—kipindupindu (cholera), homa...

magonjwa2 days ago

Magonjwa 5 ya MOYO yanayoweza Kuua haraka

Magonjwa ya moyo na mishipa ni miongoni mwa sababu kubwa za vifo duniani. WHO inaeleza kuwa magonjwa ya moyo na...

FEATURES3 days ago

Rubani Asimulia Jinsi Alivyopambana Baada ya Kuchomwa Kisu na Rubani Mwenza Kwenye Ndege ya Flydubai

Rubani wa ndege ya Flydubai, Captain Smit Machchhar, amesimulia tukio la kutisha lililotokea ndani ya chumba cha marubani baada ya...

Hospital3 days ago

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku, hali inayodhihirisha ukubwa wa tatizo...

Utafiti3 days ago

Maambukizi Yanayozuilika Yasababisha Moja Kati ya Kesi Nane za Saratani Duniani

Utafiti mpya wa Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC), ambalo ni sehemu ya Shirika la Afya Duniani (WHO),...

166
0