Dalili za Ugonjwa wa AMIBA ni Zipi?

Dalili za Ugonjwa wa AMIBA ni Zipi?

• • • • •

UGONJWA WA AMIBA(chanzo,dalili na Tiba yake)

Huu ni ugonjwa unaohusu utumbo mpana wa binadamu kushambuliwa na vimelea vya magonjwa ambavyo kwa kitaalam hujulikana kama Amoeba.

CHANZO CHA UGONJWA WA AMIBA

Hivo basi, chanzo cha ugonjwa wa amiba ni mashambulizi ya vimelea vya amiba hasa hasa jamii ya Entamoeba histolytica.

Vimelea hivi huingia moja kwa moja kwenye mwili wa binadamu kwa kupitia mdomoni na kuenda moja kwa moja kwenye njia ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula mpaka kufika kwenye utumbo mkubwa.

DALILI ZA UGONJWA WA AMIBA NI PAMOJA NA;

- Mgonjwa kuanza kupata maumivu ya tumbo sana mithili ya tumbo kusokota

- Mgonjwa kuanza kujisaidia choo kilaini sana

- Wakati mwingine Mgonjwa kujisaidia kinyesi cha rangi ya kijani, kinyesi chenye vitu kama makamasi n.k

- Mgonjwa kuharisha au kujisaidia haja kubwa ya maji maji sanaa

- Mgonjwa kujisaidia kinyesi ambacho kimechanganyika na damu

- Mgonjwa kutoa hewa kwa njia ya haja kubwa mara kwa mara(kujamba)

- Mgonjwa kupata maumivu ya tumbo,Kifua na viungo mbali mbali vya mwili

- Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na Homa

- Mgonjwa kupatwa na tatizo la kupungukiwa na damu

- Kupoteza appetite ya chakula kabsa

- Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefu chefu pamoja na kutapika

- Mgonjwa kupungua uzito wa mwili na kukonda

KUMBUKA; Moja ya njia ya mtu kupata vimelea hivi vya amoeba ambavyo husababisha ugonjwa huu wa amiba ni pamoja na kunywa maji machafu sana.

Maji ambayo yamechanganyika ma kinyesi cha mtu ambaye alikuwa na vimelea hivi vya amoeba.

MATIBABU YA UGONJWA WA AMIBA

Zipo dawa mbali mbali ambazo hutumika kutibu ugonjwa huu wa amiba, na dawa hizo ni kama vile; Tinidazole pamoja na Metronidazole

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!