EVENTS
MUHIMBILI yakutana na wananchi na watoto waliowahi kuugua saratani na kupona kabisa
MUHIMBILI yakutana na wananchi na watoto waliowahi kuugua saratani na kupona kabisa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jana Septemba 23, 2026, imekutana na wananchi na watoto waliowahi kuugua saratani na kupona kabisa, kwa lengo la kuwapongeza na kuwashukuru wadau mbalimbali wanaofanikisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Bi. Prissila Kinyamagoha, ameiomba jamii kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara, akisisitiza kuwa saratani ikigundulika mapema inatibika na kupona kabisa.
Bi. Prissila amewapongeza na kuwashukuru kwa dhati wazazi waliokusanya uvumilivu mkubwa katika kipindi chote cha matibabu ya watoto wao hadi kufikia hatua ya kupona.
Alibainisha kuwa ushuhuda na ujasiri wa mashujaa hao waliopona unatoa matumaini mapya kwa jamii na kusaidia kuondoa hofu pamoja na dhana potofu zilizopo nchini kuhusu matibabu ya saratani.
Aidha, uongozi wa Muhimbili umetoa shukrani za kipekee kwa wadau wote wanaoendelea kufadhili matibabu ya ugonjwa huo, huku ukitoa wito kwa wafadhili zaidi kujitokeza kuunga mkono jitihada hizo.
Yalielezwa kuwa mahitaji ya matibabu bado ni makubwa kutokana na idadi ya wagonjwa wapya kuongezeka kila siku, hivyo ushirikiano wa wadau ni nguzo muhimu katika kuokoa maisha ya Watanzania wengi zaidi. Via @itvtz
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass, Kama unachangamoto yoyote ya kiafya; Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatsApp, Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaUshauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)