Ebola
Kasi ya Ugonjwa wa Ebola ni kubwa kuliko mwitikio
Kasi ya Ugonjwa wa Ebola ni kubwa kuliko mwitikio
Akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani siku ya Jumatano Julai 29 kutokea Bunia jimboni Ituri, Mratibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola Julien Harneis amegusia kasi ya ugonjwa akisema.
«Katika saa 24 zilizopita watu 15 wamekufa kwa Ebola DRC na idadi ya wagonjwa inaongezeka kwa kasi, ikiwa ni maradufu katika kila siku 20. Kasi ya ongezeko ni kubwa kuliko kasi yetu ya mwitikio.”
Amezungumzia pia watoa huduma wanaosaidia harakati za kudhibiti ebola akisema,
“Lakini nimeshuhudia pia kazi ya kipekee ya watu kwenye jamii kama Grace na Christine wanaopika chakula cha WFP kwa ajili ya wagonjwa walioko kwenye vituo karibu na nyumbani kwao. Pia wahudumu wa kujitolea kwa Msalaba MWekundu wanaozika waliofariki dunia, vile vile wauguzi, madaktari na wakongomani kutoka bara la Afrika na kote duniani. »
Credits: Source UN(Umoja wa Mataifa)
