Connect with us

Ebola

Majaribio ya chanjo yameanza DR Kongo kutathmini kinga dhidi ya Ebola

Avatar

Published

on

Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema majaribio ya chanjo nchini DR Kongo yanatoa matumaini ya kupata kinga dhidi ya Ebola ya aina ya Bundibugyo.Picha: Denis Balibouse/REUTERS

Majaribio ya chanjo yameanza DR Kongo kutathmini kinga dhidi ya Ebola

Majaribio ya chanjo yameanza DR Kongo kutathmini kinga dhidi ya Ebola ya Bundibugyo, ambayo haina chanjo iliyoidhinishwa. Mlipuko huo umesababisha zaidi ya maambukizi 9,700 na vifo zaidi ya 4,600.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeanza majaribio ya chanjo katika juhudi za kukabiliana na mlipuko mbaya zaidi wa Ebola kuwahi kuikumba nchi hiyo. Utafiti huo unalenga kubaini ikiwa chanjo zinaweza kuzuia maambukizi ya virusi vya aina ya Bundibugyo.

Washiriki wa kwanza walichanjwa Ijumaa, Oktoba 23, mjini Bunia, makao makuu ya jimbo la Ituri kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Eneo hilo ndilo kitovu cha mlipuko ambao umesababisha zaidi ya maambukizi 9,700 na vifo zaidi ya 4,600.

Majaribio hayo, yaliyopewa jina la Tumaini, yameanza kwa kutumia chanjo ya Ervebo. Chanjo hiyo tayari imeidhinishwa dhidi ya virusi vya Ebola vya aina ya Zaire, lakini uwezo wake wa kutoa kinga dhidi ya Bundibugyo bado haujathibitishwa.

Kutokuwepo kwa chanjo au dawa maalumu iliyoidhinishwa dhidi ya Bundibugyo ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazokabili juhudi za kudhibiti mlipuko huo. Majaribio haya yanalenga kutoa ushahidi wa kisayansi kuhusu usalama na ufanisi wa chanjo zinazochunguzwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema sayansi inatoa matumaini. Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, amesema WHO inaunga mkono juhudi hizo zinazoongozwa na Kongo kutafuta majibu na kuokoa maisha.

Je, Ervebo inaweza kutoa kinga?
Ingawa Ervebo hutumika dhidi ya Ebola ya aina ya Zaire, haiwezi kudhaniwa kuwa inatoa kinga sawa dhidi ya Bundibugyo. WHO inasema ushahidi uliopo kuhusu uwezo wake wa kukinga dhidi ya aina nyingine za virusi vya Ebola bado ni mdogo na haujatoa jibu la uhakika.

Kwa hiyo, watafiti watachunguza ikiwa chanjo hiyo inaweza pia kuwalinda watu walio katika hatari ya kuambukizwa Bundibugyo. Kuanza kwa majaribio hakumaanishi kwamba ufanisi huo tayari umethibitishwa.

Utafiti utatumia mbinu ya kuwachanja watu walio katika mzunguko wa mawasiliano wa wagonjwa, hasa wanaoonekana kuwa katika hatari kubwa ya maambukizi. Lengo ni kutathmini kinga kwa watu wanaoweza kukutana na virusi wakati mlipuko ukiendelea.

Mfumo wa majaribio ya Tumaini umeandaliwa kuruhusu chanjo kadhaa kutathminiwa katika utafiti mmoja. Watafiti wataangalia usalama wake, uwezo wa kuchochea mwitikio wa kinga mwilini na ufanisi wa kuzuia ugonjwa.

Chanjo nyingine mbili zinaandaliwa
Mbali na Ervebo, chanjo mbili zinazotengenezwa mahsusi dhidi ya Bundibugyo zinatarajiwa kuingizwa katika majaribio hayo baada ya kuendelea katika tafiti ndogo za awali.

Moja inatengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford na hutumia teknolojia ya ChAdOx1, inayotegemea kirusi kilichobadilishwa kubeba maelekezo ya kuchochea kinga mwilini. Nyingine inatengenezwa na kampuni ya Moderna ya Marekani kwa kutumia teknolojia ya mRNA.

Chanjo hizo zimepata ufadhili kutoka Muungano wa Ubunifu wa Maandalizi dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko, CEPI. Muungano huo unasema zinatarajiwa kujiunga na utafiti wa Tumaini hivi karibuni.

Majaribio yatawahusisha pia wajawazito na watoto wenye umri wa miaka 12 na kuendelea. Hilo litasaidia kukusanya ushahidi kuhusu makundi ambayo mara nyingi hayajumuishwi katika tafiti za chanjo. Via:#DW

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

Utafiti23 hours ago

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka Vinavyosababishwa na Magonjwa ya Moyo na Kiharusi – Utafiti...

Afya News1 day ago

Mtoto Afariki Dunia kwa Surua Marekani, Vifo 3 Vyaripotiwa Wiki Hii

Mtoto mchanga afariki dunia kutokana na surua nchini Marekani, vifo vitatu vyaripotiwa wiki hii Mtoto mchanga nchini Marekani amefariki dunia...

CHANJO1 day ago

Chanjo Mbili Mpya za Ebola Kuongezwa kwenye Majaribio ya Kitabibu Huku Utafiti wa Tiba Ukiendelea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya ugonjwa wa Ebola zinatarajiwa kuongezwa kwenye...

Afya News2 days ago

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke. Bodi ya Dawa na Sumu...

magonjwa2 days ago

Sababu ya mikono kufa ganzi

Sababu 12 Za Mikono Kufa Ganzi: DALILI HII INASABABISHWA NA NINI? Mikono kufa ganzi ni hali ambayo mtu hupoteza hisia...

Uzazi&Ujauzito3 days ago

Kubeba mimba baada ya kujifungua

Kubeba mimba baada ya kujifungua JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano...

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio...

Utafiti5 days ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini Kenya, ikiwasaidia wauguzi na...

afyatips5 days ago

Upungufu wa Vitamini D,Dalili Zake, Visababishi na Madhara Ambayo Unaweza Usiyatambue Mapema

Patient Story Via BBC;Sikujua nilikuwa na upungufu wa vitamini D hadi nilipozirai kazini’ Msichana mwenye umri wa miaka 23, Saskia...