Connect with us

Ebola

Daktari kijana nchini DRC, Victor Kingombe, amefariki dunia kwa Ebola

Avatar

Published

on

Daktari kijana nchini DRC, Victor Kingombe, amefariki dunia kwa Ebola

Daktari kijana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Victor Kingombe, amefariki dunia kwa maambukizi ya virusi vya Ebola katika kituo cha matibabu mjini Kisangani, alipokuwa akihudumu.

Aidha, Wafanyakazi wenzake wa afya na wanafamilia walihudhuria mazishi yake, huku timu maalumu ikiwa imevaa mavazi ya kujikinga wakati wa kuuhamisha mwili wake.

Kifo cha daktari huyo kimetokea wakati maambukizi ya Ebola yakiongezeka katika baadhi ya maeneo nje ya kitovu cha mlipuko.

Ingawa maambukizi yamepungua katika mkoa wa Ituri, Kivu Kaskazini imeripoti ongezeko la asilimia 73 ndani ya wiki tatu.

Kwa upande wake, Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuhusu kuenea kwa ugonjwa huo kutokana na changamoto za kiusalama, uhamaji wa wananchi, migomo ya wafanyakazi wa afya na mwingiliano mkubwa wa watu.

Makamu Gavana wa Tshopo, Didier Lomoyo Iteku, amesema kifo cha daktari huyo ni ushahidi kwamba Ebola ni ugonjwa wa kweli na amewataka wananchi kuamini huduma za afya.

Hata hivyo, Serikali ilianza kuwapatia chanjo ya Ervebo wafanyakazi wa afya mjini Kisangani mwezi Agosti, huku tafiti za matibabu mapya zikiendelea.

Chanzo: Africa News

Afyaclass
Jukwaa la Afya na Elimu
Pata Ushauri wa Kibinafsi wa Daktari
Je, unahitaji mwongozo wa afya? Wasiliana nasi kupitia WhatsApp kwa haraka au Call,Sms +255758286584.
✚

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

Mchakato Wetu wa Ukaguzi na Uhariri (Our Review Process)

✔ Ilipitiwa na Kukaguliwa Kitiba.

Ilisasishwa mwaka @2026.

Fahamu zaidi kuhusu Maktaba ya Afya na mchakato wetu wa uhariri(Review Process).

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

Afya News5 hours ago

Tanzania yatoa wito kwa nchi za Afrika kuweka mikakati ya endelevu kwenye mapambano dhidi ya Malaria

TANZANIA YATOA WITO KWA NCHI ZA AFRIKA KUWEKA MIKAKATI YA ENDELEVU KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA Na John Mapepele, WAF-...

Others8 hours ago

Zaidi ya watu 40 wanaripotiwa kufariki dunia baada ya boti kuzama Ziwa Tanganyika

Zaidi ya watu 40 wanaripotiwa kufariki dunia baada ya boti iliyokuwa ikisafiri kutoka Kigoma nchini Tanzania kuelekea Kalemie, Jamhuri ya...

magonjwa ya ngozi9 hours ago

Mabaka Meu‌pe Kwenye Ngozi: Sababu, Dalili, Uchunguzi na Matibabu

Mabaka Meu‌pe Kwenye Ngozi: Sababu, Dalili, Uchunguzi na Matibabu Mabaka meupe kwenye ngozi ni hali ambayo sehemu fulani ya ngozi...

Ebola9 hours ago

Daktari kijana nchini DRC, Victor Kingombe, amefariki dunia kwa Ebola

Daktari kijana nchini DRC, Victor Kingombe, amefariki dunia kwa Ebola Daktari kijana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Victor...

Afya ya Akili9 hours ago

Tatizo la Afya ya Akili,Leo tuzungumze kuhusu tatizo la afya ya akili

Tatizo la Afya ya Akili Afya ya akili ni sehemu muhimu ya afya ya mtu kwa ujumla. Kwa mujibu wa...

Uzazi&Ujauzito12 hours ago

Tatizo la Ugumba Kwa Wanaume

Ugumba ni changamoto ya kupata ujauzito licha ya wanandoa kufanya tendo la ndoa bila kutumia njia za kuzuia mimba kwa...

Uzazi&Ujauzito1 day ago

Mambo haya Mama anayenyonyesha huweza kuyapitia

Mambo ambayo mama anayenyonyesha huweza kuyapitia kwenye Kipindi hiki. Fahamu kipindi Mama ananyonyesha Mtoto, Mwili wa mama hutoa maziwa kila...

EVENTS2 days ago

MUHIMBILI yakutana na wananchi na watoto waliowahi kuugua saratani na kupona kabisa

MUHIMBILI yakutana na wananchi na watoto waliowahi kuugua saratani na kupona kabisa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jana Septemba 23,...

DAWA2 days ago

Dawa ya kudhibiti pombe sasa ni rasmi kutumika

Dawa ya kudhibiti pombe sasa ni rasmi kutumika Bohari ya Dawa (MSD) imefanikiwa kuingiza shehena ya kwanza ya dawa ya...

magonjwa2 days ago

Madhara ya malaria,Fahamu hapa madhara ya Ugonjwa wa Malaria

Madhara ya Ugonjwa wa malaria Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea aina ya Plasmodium na huenezwa hasa kwa kuumwa na...

458
0