Connect with us

Others

Ikiwa ugonjwa hauambukizi, kunyonyesha ni salama

Doctor Ombeni

Published

on

Ikiwa ugonjwa hauambukizi, kunyonyesha ni salama


Grace Mhando, Mtaalamu wa lishe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili nchini Tanzania.

Zipo dhana na imani potofu mbalimbali kuusu unyonyeshaji maziwa kwa mtoto. Lakini pia iko hofu miongoni mwa jamii kuhusu mama mwenye changamoto za kiafya umnyonyesha mtoto wake iwe kwa njia ya moja kwa moja au kwa njia ya chupa.

Ingawa Wiki ya Kimataifa ya Unyonyeshaji maziwa ya mama inayoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, imefika tamati Agosti 7, lakini elimu kuhusu suala hili muhimu kwa ustawi wa binadamu ni elimu endelevu kwani kila wakati mahali fulani duniani anapatikana mama mpya.

Selina Sylivester, Afisa Muuguzi anayewapokea wanawake wajawazito na wanaonyonyesha katika hospitali yenye historia ya zaidi ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwake, Hospitali ya Taifa Muhimbili anaeleza kuhusu baadhi ya imani potofu wanazokutana nazo kuhusu unyonyeshaji.

“Unakutana na akina mama ambao wananyonyesha lakini wanakuwa na imani zao kutoka walikotoka kwamba mimi siwezi kunyonyesha mtoto au kukamua maziwa kumnywesha mtoto kwasababu niña ugonjwa labda kama Kisukari, Shinikizo la Damu, kwa hiyo anaamini kwamba akimnyinyesha mtoto akiwa na magonjwa kama hayo ataumia zaidi au kama ni shinikizo la damu itaongezeka badala ya kukaa katika hali ya kawaida.”

Madhali ugonjwa hauambukizi, kunyonyesha ni salama

Afisa Muuguzi, Selina Sylivester anaeleza kwamba wanawaondoa wasiwasi akina mama hao kuwa hata ukiwa na hali hizo za magonjwa sugu kama kisukari na shinikizo la damu unanyonyesha kama kawaida.

Rachel Chalo kabla ya kujifungua aligundulika kuwa ana ugonjwa wa Kisukari, shinikizo la damu na pumu. Mama huyu ambaye amepata mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati lakini anaendelea vizuri sana anathibitisha yaliyosemwa na Afisa Muuguzi hapo awali kuwa licha ya changamoto za kiafya za mama kuangaliwa kwa ukaribu, lakini pia kipaumbele kinaelekezwa katika kuhakikisha mtoto ananyonya maziwa ya mama angalau miezi sita ya mwanzo.

Maziwa ya ng’ombe je?

Lakini kuna sababu gani hasa ya kuhangaika hivi ikiwa pia kuna maziwa ya wanyama kama ng’ombe? Grace Mhando ni mmoja wa Maafisa Lishe wa wa Hospitali ya Muhimbili analifafanua hili kitaalamu akisema, “maziwa ya mama ni bora zaidi kuliko maziwa ya ng’ombe kwasababu maziwa ya mama yana virutubisho  vya kinga vinavyomkinga mtoto dhidi ya magonjwa.” Mtaalamu huyo wa lishe anaeleza zaidi kuwa pia maziwa ya mama yana maji ambayo yanatosha kumfanya mtoto asihitaji kupewa maji ya kawaida.

Vipi kuhusu lishe ya mama mwenyewe? Afisa Lishe Grace Mhando anatoa ushauri kwamba mama mnyonyeshaji inabidi ale vyakula mbalimbali ambavyo ni salama na muhimu katika mwili, anywe maji ya kutosha, kufanya mazoezi na kupumzika vya kutosha ili kuufanya ubongo ufanye kazi yake vizuri kuzalisha maziwa ya kutosha.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

WHO2 days ago

Kutokomeza Magonjwa yaliyosahaulika ya Kitropiki Duniani

Mafanikio Na Changamoto Katika Kutokomeza MAGONJWA YALIYOSAHAULIKA YA KITROPIKI DUNIANI Magonjwa yaliyosahaulika ya kitropiki (Neglected Tropical Diseases – NTDs) ni...

Utafiti3 days ago

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka Vinavyosababishwa na Magonjwa ya Moyo na Kiharusi – Utafiti...

Afya News3 days ago

Mtoto Afariki Dunia kwa Surua Marekani, Vifo 3 Vyaripotiwa Wiki Hii

Mtoto mchanga afariki dunia kutokana na surua nchini Marekani, vifo vitatu vyaripotiwa wiki hii Mtoto mchanga nchini Marekani amefariki dunia...

CHANJO3 days ago

Chanjo Mbili Mpya za Ebola Kuongezwa kwenye Majaribio ya Kitabibu Huku Utafiti wa Tiba Ukiendelea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya ugonjwa wa Ebola zinatarajiwa kuongezwa kwenye...

Afya News4 days ago

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke. Bodi ya Dawa na Sumu...

magonjwa4 days ago

Sababu ya mikono kufa ganzi

Sababu 12 Za Mikono Kufa Ganzi: DALILI HII INASABABISHWA NA NINI? Mikono kufa ganzi ni hali ambayo mtu hupoteza hisia...

Uzazi&Ujauzito5 days ago

Kubeba mimba baada ya kujifungua

Kubeba mimba baada ya kujifungua JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano...

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio...

Utafiti7 days ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini Kenya, ikiwasaidia wauguzi na...