Connect with us

Uzazi&Ujauzito

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

Doctor Ombeni

Published

on

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA?

Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada ya kujifungua kabla haujapata mzunguko mwingine wa hedhi. Hii ni kwa sababu, yai la mwanamke huwa linapevuka wiki mbili kabla ya kupata hedhi, yaani siku ya kumi na nne kabla ya tarehe ya kwanza ya kupata hedhi, 

kwa maana hiyo yai linaweza kupevuka na kuweza kuwa kwenye hatari ya kupata ujauzito bila wewe kutambua. Kwa sababu, kupata kwa hedhi ni matokeo ya yai kutopevushwa.

Kimsingi, ni ngumu kwa mama mjamzito kupata mimba mara tu baada ya kujifungua, hasa kama unanyonyesha vizuri.

Hii ni kwa sababu, kuna vichocheo au homoni ambazo hutolewa kipindi cha kunyonyesha ambayo huzuia yai kupevuka kwa yai na kusababisha kukosa hedhi kwa miezi kadhaa, kitaalamu lactational Amenorrhea. 

Kukosa huku hedhi hakukukingi kwa asilimia mia moja kupata ujauzito ndio maana ukijifungua kwenye vituo vya afya au hospitali huwa unashauriwa kuhusu njia bora za uzazi wa mpango pale utakapokuwa tayari kuanza tena kufanya tendo la ndoa.

Wakina mama wengi huwa wanapenda kusubiri kupewa ruhusa na daktari wake wakati wanapoenda kliniki baada ya kujifungua, ingawa wapo ambao huwa wanajisikia wako tayari pale tu damu inapokata au nyuzi na michubukuko ya kupindi cha kujifungua vinapopona.

Kama unanyonyesha na kutumia maziwa ya kopo, hedhi inaweza kurudi baada ya wiki sita mpaka kumi baada ya mtoto kuzaliwa. 

Kama ni kunyonyesha peke yake inaweza kuchukua kipindi kirefu Zaidi yaani miezi kadhaa, ingawa hamna jibu la moja kwa moja kuhusu  ni lini au ni kipindi kipi unaweza kupata hedhi.

Ni vyema kupata ushauri wa daktari hata kama ni siku za awali baada ya kujifungua, ili kuweza kupanga mapema na kuamua.

Je naweza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango wakati nanyonyesha?

Katika miezi sita ya mwanzo huwa haishauriwi kutumia vidonge vya uzazi wa mpango vyenye mchanganyiko wa homoni au vichocheo kwa maana huweza kupunguza kiasi cha maziwa ambacho hutolewa. Ingawa kutumia kidonge chenye kichocheo aina moja kitaalamu Progesterone only pill huwa ni salama kabisa. 

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio...

Utafiti1 day ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini Kenya, ikiwasaidia wauguzi na...

magonjwa1 year ago

Kuhisi vitu vinatembea mwilini,chanzo chake na Tiba

Kuhisi vitu vinatembea mwilini,chanzo chake na Tiba Hali hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini kwa kitaalam hujulikana kama Formication Baadhi ya watu...

WHO3 days ago

Barbados yafanikiwa Kuzuia Maambukizi ya VVU Kutoka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto

Barbados yafanikiwa Kuzuia Maambukizi ya VVU Kutoka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa Barbados...

Uzazi&Ujauzito2 years ago

Dalili za hatari kwa mama mjamzito

Dalili za hatari kwa mama mjamzito ni zipi Moja ya Vitu ambavyo Wakina mama Wajawazito hupewa ELIMU wanapohudhuria kliniki kuanzia...

magonjwa ya wanaume4 days ago

Madhara ya kupiga puchu,madhara ya kupiga nyeto, kwa Wanaume

Madhara ya kupiga puchu,madhara ya kupiga nyeto, kwa Wanaume Madhara ya punyeto kwa Wanaume,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo Tabia...

Story4 days ago

Wanandoa wa Nigeria Wapata Mtoto wa Kwanza Baada ya Miaka 19 ya Kusubiri

Wanandoa wa Nigeria Wapata Mtoto wa Kwanza Baada ya Miaka 19 ya Kusubiri Wanandoa kutoka nchini Nigeria wameibua hisia za...

EVENTS4 days ago

Siku ya Lishe Kitaifa 26-30 Oktoba, 2026 Imarisha afya yako kwa kuchagua nafaka zisizokobolewa

Siku ya Lishe Kitaifa 26-30 Oktoba, 2026 Imarisha afya yako kwa kuchagua nafaka zisizokobolewa. CHAGUA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA IMARISHA AFYA YAKO!...

magonjwa ya watoto4 days ago

Kitovu cha Mtoto:muunganisho muhimu kati ya mama na mtoto wakati wa ujauzito

Kitovu cha Mtoto:muunganisho muhimu kati ya mama na mtoto wakati wa ujauzito Kitovu cha Mtoto (Umbilical cord) ni mojawapo ya...