Others
Zaidi ya watu 40 wanaripotiwa kufariki dunia baada ya boti kuzama Ziwa Tanganyika
Zaidi ya watu 40 wanaripotiwa kufariki dunia baada ya boti iliyokuwa ikisafiri kutoka Kigoma nchini Tanzania kuelekea Kalemie, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kuzama katika Ziwa Tanganyika. Watu wengine 49 wameokolewa.
Boti hiyo iliyokuwa imebeba abiria pamoja na shehena ya mizigo, ilizama karibu na Kijiji cha Mapera, upande wa DRC. Taarifa zinaeleza kuwa karibu watu 100 walikuwa ndani ya chombo hicho wakati wa ajali, huku shughuli za uokoaji na utafutaji zikiendelea kuwatafuta watu ambao hawajapatikana.
Ajali hiyo imetokea Alhamisi, Septemba 24, 2026, wakati boti hiyo ikielekea Kalemie kutoka Kigoma. Chanzo cha ajali bado hakijathibitishwa rasmi, ingawa taarifa za awali kutoka eneo la tukio zimeeleza kuwa mzigo mkubwa uliokuwa kwenye boti hiyo umeibua maswali kuhusu chanzo cha ajali.
Source:ITVDigital
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari HapaMchakato Wetu wa Ukaguzi na Uhariri (Our Review Process)
Ilisasishwa mwaka @2026.
Fahamu zaidi kuhusu Maktaba ya Afya na mchakato wetu wa uhariri(Review Process).
