Connect with us

magonjwa ya wanaume

Tatizo la hydrocele,chanzo,dalili na Tiba yake

Doctor Ombeni

Published

on

Tatizo la hydrocele,chanzo,dalili na Tiba yake

Hydrocele ni tatizo ambalo huhusisha kuvimba kwa eneo la korodani au uvimbe ndani ya vifuko vya korodani(Scrotum) unaosababishwa na kujaa maji.

Tatizo hili ndyo kwa jina Lingine hujulikana kama “BUSHA”.

Tatizo la hydrocele ni aina ya uvimbe kwenye korodani, au mfuko wa ngozi unaoshikilia korodani. Uvimbe huu hutokea wakati majimaji yanapojikusanya kwenye kifuko chembamba kinachozunguka korodani. Hydroceles ni kawaida pia kwa watoto wachanga”

Dalili za Tatizo la hydrocele

Mara nyingi ishara pekee ya hydrocele ni uvimbe usio na uchungu au maumivu kwenye korodani moja au zote mbili.

Uvimbe huo unaweza kufanya korodani ya mtu mzima kuhisi nzito. Kwa ujumla, maumivu yanaongezeka wakati uvimbe unaongezeka. Wakati mwingine, eneo lenye kuvimba linaweza kuwa dogo asubuhi na kubwa baadaye mchana.

Vitu hivi huongeza hatari ya Kupata tatizo la hydrocele

Hydroceles nyingi zipo wakati wa kuzaliwa. Tafiti zinaonyesha Angalau asilimia 5% ya wanaume waliozaliwa wana hydrocele,

Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, ambao huzaliwa zaidi ya wiki tatu kabla ya tarehe zao za kuzaliwa, wana hatari kubwa ya kuwa na hydrocele pia.

Sababu za hatari za kupata hydrocele baadaye maishani ni pamoja na:

  • Kupata Jeraha au kuvimba ndani ya korodani.
  • Maambukizi, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya zinaa.n.k

Madhara ya tatizo la Hydrocele ni yapi?

Mara nyingi si tatizo lenye hatari kubwa au madhara zaidi ni la kawaida, Na pia haliathiri uwezo wa kupata mtoto kama baadhi ya watu wanavyosema.

Ingawa pia hydrocele inaweza kuhusishwa na shida za kiafya ambazo zinaweza kusababisha madhara makubwa. Kuna uhusiano wa hydrocele na Matatizo haya:

• Maambukizi au tumor.

Na matokeo yake inaweza kusababisha korodani kutengeneza kiwango kidogo cha manii au zisifanye kazi vizuri kama kawaida.

• Hernia ya inguinal.

Hii inaweza kusababisha matatizo ya kiafya ambayo huweza kutishia maisha.

Chanzo cha tatizo la hydrocele

Tatizo la hydrocele au Busha ni tatizo la kujaa kwa maji kwenye mfuko wa korodani za mwanaume.

SABABU AU CHANZO CHA TATIZO LA HYDROCELE NI NINI?

Tatizo la Busha au hydrocele huweza kusababishwa na vitu mbali mbali ikiwemo;

– hali ya eneo la Kuzunguka Korodani kuwa na Maji mengi kuliko ilivyokawaida,

– Mirija ya Lymph kwenye Korodani au mishipa ya Damu inayosafirisha damu kutoka kwenye korodani kwenda maeneo mengine ikiwa Imeziba kabsa,

Vyote hivi hupelekea kupungua kwa ufyonzwaji wa maji yanayozunguka eneo la korodani. Hali ambayo hupelekea maji kujikusanya kwenye vifuko vya Korodani.

HIZI NI BAADHI YA SABABU ZA MAJI KUWA MENGI KWENYE ENEO LA KORODANI

• Mtu kupata Majeraha au kuumia kwenye Korodani(Injury)

• Mtu kupata Maambukizi ya magonjwa kwenye eneo la Korodani

• Mtu kupata Maambukizi kwenye mshipa wa-epididymis

• Mtu kupata Maambukizi yanayo sababishwa na vimelea wa filaria (filariasis) wanao sababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.

• Mtu kupata tatizo la Korodani Kujisokota ambapo kwa kitaalam hujulikana kama testicular torsion

• Mtu kupata Uvimbe kwenye korodani yaani testicular tumors,

Hii pia huweza kuchangia uzalishwaji wa maji mengi kwenye korodani.

• Mtu Kufanyiwa upasuaji ambao huweza kuathiri ufyozwaji wa maji kwenye korodani

• Mtu kupata Tiba ya mionzi kipindi cha nyuma. n.k

KUMBUKA; Watu ambao wapo maeneo ya Pwani, wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la Busha,

Hui ni kutokana na kuwa kwenye hatari zaidi ya kung’atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!

References;

  1. Mayo Clinic (2025). Hydrocele: Symptoms and Causes.
    Chanzo hiki kinaeleza maana ya hydrocele, dalili, sababu na wakati wa kumuona daktari.
  2. Cleveland Clinic (2023). Hydrocele: Causes, Symptoms, Diagnosis & Treatment.
    Kinaeleza visababishi, vipimo, matibabu na madhara yanayoweza kutokea.
  3. National Center for Biotechnology Information (NCBI Bookshelf). Hydrocele – StatPearls.
    Chanzo cha kitaalamu kinachofafanua aina za hydrocele, uchunguzi, visababishi na matibabu.
  4. Mayo Clinic (2025). Hydrocele: Diagnosis and Treatment.
    Kinaeleza namna hydrocele inavyogunduliwa na chaguo za matibabu, ikiwemo upasuaji.
  5. British Association of Urological Surgeons (BAUS) (2024). Repair of a Scrotal Hydrocele.
    Mwongozo wa kitaalamu unaofafanua upasuaji wa hydrocele, uangalizi bila upasuaji na changamoto za kutoa maji kwa sindano.
✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti1 day ago

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Sophia MD's Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila...

Afya News1 day ago

Mtoto Afariki Dunia kwa Surua Marekani, Vifo 3 Vyaripotiwa Wiki Hii

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Sophia MD's Mtoto mchanga afariki dunia kutokana na surua nchini Marekani, vifo...

CHANJO1 day ago

Chanjo Mbili Mpya za Ebola Kuongezwa kwenye Majaribio ya Kitabibu Huku Utafiti wa Tiba Ukiendelea

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Sophia MD's Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo mbili mpya...

Afya News2 days ago

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Sophia MD's Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya...

magonjwa2 days ago

Sababu ya mikono kufa ganzi

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Sophia MD's Sababu 12 Za Mikono Kufa Ganzi: DALILI HII INASABABISHWA NA...

Uzazi&Ujauzito3 days ago

Kubeba mimba baada ya kujifungua

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Sophia MD's Kubeba mimba baada ya kujifungua JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA...

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Sophia MD's JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Sophia MD's TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili...

Utafiti5 days ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Sophia MD's Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu...

afyatips5 days ago

Upungufu wa Vitamini D,Dalili Zake, Visababishi na Madhara Ambayo Unaweza Usiyatambue Mapema

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Sophia MD's Patient Story Via BBC;Sikujua nilikuwa na upungufu wa vitamini D...