Connect with us

News

TANZIA;Miili saba wanafunzi yaopolewa Arusha

Avatar photo

Published

on

Miili saba wanafunzi yaopolewa Arusha

Arusha. Miili saba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ghati Memorial iliyoko Murieti jijini Arusha imepatikana katika maeneo tofauti na kukamilisha idadi ya wanafunzi waliokufa maji katika ajali hiyo.

Miii hiyo imepatikana kwa msaada wa uokozi unaofanywa na Jeshi la Zimamoto, Polisi kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya pamoja na wananchi.

Wanafunzi hao wamefariki dunia baada ya gari la shule waliokuwemo kuangukia kwenye korongo lililojaa maji eneo la Dampo mkoani Arusha, saa 12 asubuhi ya leo April 12, 2024.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Arusha, Osward Mwanjejele amesema gari hilo lilitumbukia kwenye korongo linalomwaga maji yake katika mto mkubwa wa Themi.

“Kwa taarifa za awali zinasema kuwa gari lilikuwa na wanafunzi 11 na walimu wawili na dereva na hapo hapo walisaidiwa wanafunzi wanne,mwalimu na dereva,” amesema.

Mashuhuda wa ajali hiyo, Evance Rafaeli amesema gari hilo linapita kila siku asubuhi kuchukua wanafunzi katika kaya mbalimbalikuwapeleka shule, lilipita asubuhi kufuata wanafunzi, lakini wakati linarudi lilikuta maji yamejaa na kutokea ajali hiyo.

“Tulisikia kelele za mama mmoja hapa jirani na kijiwe chetu cha kufyatua matofali na katika kukimbia ndio tukaona gari la wanafunzi likielea juu ya maji, akasema alimuonya dereva huyo asipite maji ni mengi, lakini akawa mbishi akajaribu kupita kabla maji hayajamzidi nguvu na gari kuporomokea korongoni,”amesema Rafaeli.

Amesema walianza kazi ya kuokoa na walifanikiwa kutoa watu wawili wazima ambao ni mwalimu na dereva pamoja na wanafunzi watatu wakiwa hai, huku mmoja wa kiume akiwa ameshafariki baada ya gari kujaa maji.

Lilian Mussa amesema alifika eneo la tukio na kukuta kazi ya kuokoa watu likifanywa na watu wawili ambao walilazimika kupiga kelele za kuomba msaada, hivyo watu waliokuwapo barabarani walikwenda kusaidia kabla ya gari kuendelea kusogea na watoto wengine wakionekana kusombwa na maji.

Mmoja wa wananchi walioko kwenye timu ya uokoaji, Elia Mbise amesema wamefanikiwa kuopoa mwili wa mtoto mwingine eneo la Muriet, saa sita mchana kabla ya saa 7:15 kuopoa mwili mwingine eneo la Miongoine.

“Kinachotusaidia ni kufuata nguo ambazo huku korongoni tunapopita tunaziona zimekwama kwenye miti ndio tunaokota, lakini tulipofika eneo la Muriet tuliona pia koti katika kuokota kuvuta ndio tukaona ni mwili tukauchukua” amesema na kuongeza;

“Mbali na hilo pia wamefanikiwa kuupata mwili mwingine eneo la Mirongoine ambazo zote zinapelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti iliyoko katika Hospitali ya Muriet.”

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa amesema ajali imetokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku katika maeneo mbalimbali katika jiji la Arusha na kuelekeza maji yake katika njia mbalimbali, ikiwemo katika korongo hilo la Sinoni.

Ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Arusha kuwa watulivu wakati zoezi la uokoaji linaendelea, huku akiwataka wazazi kwenda kutambua miili ya watoto wao inayoendelea kuopolewa bila kutaja idadi.

“Tusiwe wepesi kulia na kuhukumu wote kuwa wamekufa, tusubiri hadi mwisho kikubwa wengine waende Muriet wakatambue miili ya watoto wao ambao inapatikana,” amesema.

Amesema dereva wa gari hilo amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa katika jaribio la kukimbia kabla hajadhibitiwa na wananchi waliokuwa eneo la tukio.

Karibu AfyaUpdates Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In https://afyaclass.com  Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa4 weeks ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa1 month ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa2 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa2 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa3 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake4 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa1 day ago

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 days ago

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi Madhara ya kula nyama ya ng’ombe mbichi Ni desturi ya baadhi ya watu kula...

Magonjwa1 week ago

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani Mkojo kuuma au kupata maumivu wakati wa kukojoa ni hali ambayo kwa kitaalam...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono dalili Zake

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa2 weeks ago

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu Haya ni maneno ambayo umekuwa ukiyasikia sana linapokuja swala la vipimo cha UKIMWI, je...

Magonjwa3 weeks ago

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia. Kutana na Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa unaosababishwa na konokono

Ugonjwa unaosababishwa na konokono Ugonjwa unaosababishwa na konokono unaitwa schistosomiasis, au bilharzia. Ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na minyoo wanaoitwa...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake. Wengi tumesikia kuhusu Red Eyes(Macho mekundu) Lakini je umewahi kusikia kuhusu Pink Eyes,?...

Magonjwa3 weeks ago

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapa

Omeprazole inatibu ugonjwa gani Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi...

Magonjwa4 weeks ago

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani Mate kujaa Mdomoni,ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na zipo...