Connect with us

Other posts

Ukiukwaji wa haki ya afya ya uzazi kwa wanawake wachangia vifo vinavyoweza kuzuilika: UNFPA

Avatar photo

Published

on

Ukiukwaji wa haki ya afya ya uzazi kwa wanawake wachangia vifo vinavyoweza kuzuilika: UNFPA

Wanawake wa Kiafrika wana uwezekano wa kufa mara 130 zaidi kutokana na ujauzito au matatizo ya uzazi kuliko wanawake wa Ulaya na Amerika Kaskazini, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyochapishwa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi UNFPA.

Ripoti hiyo “Maisha Yaliyounganishwa, Mizizi ya Matumaini: Kukomesha kukosekana kwa usawa katika afya na haki za ngono na uzazi”, inaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya vifo vya uzazi vinavyoweza kuzuilika hutokea katika nchi ambazo ziko katika hali ya shida au changamoto.

Pia inaangazia jukumu ambalo ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kijinsia na aina nyingine za ubaguzi huchukua katika kuzuia maendeleo kwenye masuala ya ngono na afya ya uzazi.

Kulingana na matokeo ya utafiti wa ripoti hiyo “Wanawake na wasichana waliokwama katika umaskini wana uwezekano mkubwa wa kufa mapema kutokana na ukosefu wa huduma za afya za kutosha kama wanatoka katika makundi ya wachache au wamekwama katika mazingira ya migogoro.”

Kwa ujumla, ripoti inasema kumekuwa na maendeleo makubwa katika afya ya ngono na uzazi ikawa kipaumbele cha maendeleo endelevu miongo mitatu iliyopita.

Akizindua ripoti hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Natalia Kanem amesema “Katika nafasi ya kizazi kimoja, tumepunguza kiwango cha mimba zisizotarajiwa kwa karibu theluthi moja, kupunguza kiwango cha vifo vya uzazi kwa theluthi moja, na kupata sheria dhidi ya unyanyasaji wa majumbani katika zaidi ya nchi 160.”

Mchakato uliokwama

Bi. Kanem ameongeza kuwa lakini maendeleo yanapungua au kukwama katika maeneo kadhaa muhimu.

“Katika ulimwengu ambapo robo ya wanawake hawawezi kukataa kufanya ngono na wapenzi wao na karibu mmoja kati ya 10 hawana sauti kuhusu uzazi wa mpango, wanawake 800 wanakufa kila siku wakijifungua idadi ya kutatanisha ambayo haijabadilika tangu 2016.”

Ameendelea kusema kuwa takriban vifo 500 kati ya hivyo vinavyoweza kuzuilika vinatokea kwa siku katika nchi zinazoishi zikipitia majanga ya kibinadamu na migogoro.

“Ulimwengu haujapiga hatua katika kuokoa wanawake kutokana na vifo vinavyoweza kuzuilika wakati wa ujauzito na kujifungua,” amesema Bi. Kanem, akiongeza kuwa kwa mara ya kwanza, takwimu zimekusanywa kuhusu endapo uhuru wa mwili wa wanawake unaimarika kwa wakati.

Amesema “Katika asilimia 40 ya nchi ambako taarifa zimepatikana, uhuru unadhoofika kutokana na kushindwa kuwafikia walio nyuma zaidi”.

Ripoti imebainisha kuwa kuna tofauti ya wazi kati ya mataifa ya Kaskazini na Kusini, Magharibi na Mashariki, linapokuja suala la uzazi wa mpango, huduma za uzazi salama, utunzaji wa heshima ya uzazi, na huduma zingine muhimu.

Ajnur Demir akiwa katika picha ya pamoja na familia yake wakati akihudhuria warsha ya ukosefu wa uraia iliyoungwa mkono na UNHCR huko Skopje, Macedonia Kaskazini. (Maktaba)

Suala la usawa

Hata hivyo, hata ndani ya mataifa hayo kuna “mapengo ya ukosefu wa usawa”, ripoti inasisitiza.

Wanawake wenye asili ya Kiafrika katika bara la Amerika wanakabiliwa na viwango vya juu vya vifo vya uzazi ikilinganishwa na wanawake weupe, jambo ambalo linadhihirika hasa nchini Marekani ambako ni mara tatu ya wastani wa kitaifa.

Watu wa jamii za asili na makabila madogo pia wanakabiliwa na hatari kubwa zinazohusiana na ujauzito na kujukifungua.

Ndani ya bara Ulaya, nchini Albania, kwa mfano, ripoti inasema zaidi ya asilimia 90 ya wanawake wa Kiromania kutoka makundi yaliyotengwa zaidi kiuchumi na kijamii walikuwa na matatizo makubwa katika kupata huduma za afya ikilinganishwa na asilimia 5 tu ya wanawake wa kabila la Kialbania kutoka tabaka zilizobahatika zaidi.

Zaidi ya hayo, wanawake wenye ulemavu wana uwezekano wa kufikia mara 10 zaidi wa kukabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia, na watu wenye mwelekeo tofauti wa kijinsia na kujieleza kijinsia hukumbana na ukatili mkubwa na vikwazo vya kupata huduma.

Mwanamke akiwa na mtoto wake mchanga akiwasikiliza wafanyakazi wa UNFPA katika kikao cha kuongeza uelewa kuhusu ukatili wa kijinsia katika Kituo cha One Stop katika Hospitali ya Sominé Dolo.

Hakuna suluhu moja inayokidhi haja zote 

Ripoti pia inaangazia umuhimu wa kuandaa programu kulingana na mahitaji ya jamii na kuwawezesha wanawake na wasichana kuunda na kutekeleza suluhu za kibunifu.

Pia inakokotoa kwamba ikiwa dola bilioni 79 za ziada zitawekezwa katika nchi za kipato cha chini na cha kati ifikapo mwaka 2030, mimba zisizopangwa milioni 400 zinaweza kuepukwa, maisha milioni moja yataokolewa na dola bilioni 660 katika faida za kiuchumi zinaweza kuzalishwa.

Uwezo wa kupata haki za afya ya uzazi, Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Bi. Kanem anaamini, ni changamoto nyingine kubwa akisema “Kwa hakika ni wajibu wa wanaume kuwa mabingwa wa haki za uzazi za wanawake, wa haki za uzazi za kila mtu.”

VIA: UN

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa4 weeks ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa1 month ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa2 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa2 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa3 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake4 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa1 day ago

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa2 days ago

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi Madhara ya kula nyama ya ng’ombe mbichi Ni desturi ya baadhi ya watu kula...

Magonjwa1 week ago

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani Mkojo kuuma au kupata maumivu wakati wa kukojoa ni hali ambayo kwa kitaalam...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono dalili Zake

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa2 weeks ago

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu Haya ni maneno ambayo umekuwa ukiyasikia sana linapokuja swala la vipimo cha UKIMWI, je...

Magonjwa3 weeks ago

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia. Kutana na Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa unaosababishwa na konokono

Ugonjwa unaosababishwa na konokono Ugonjwa unaosababishwa na konokono unaitwa schistosomiasis, au bilharzia. Ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na minyoo wanaoitwa...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake. Wengi tumesikia kuhusu Red Eyes(Macho mekundu) Lakini je umewahi kusikia kuhusu Pink Eyes,?...

Magonjwa3 weeks ago

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapa

Omeprazole inatibu ugonjwa gani Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi...

Magonjwa4 weeks ago

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani Mate kujaa Mdomoni,ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na zipo...