Connect with us

WHO

Zaidi ya watu 800 wafariki kwa Mpox katika bara la Afrika:WHO

Doctor Ombeni

Published

on

WHO yaripoti visa 30,000 vinavyoshukiwa kuwa vya MPOX barani Afrika, haswa nchini DRC

Takriban watu 30,000 wanaoshukiwa kuwa na virusi vya MPOX wameripotiwa barani Afrika kufikia sasa mwaka huu, wengi wao wakiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC),Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO) lilisema Jumatatu.

Zaidi ya watu 800 walikufa kwa kushukiwa kuwa na Mpox katika bara la Afrika, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilisema katika ripoti yake. 

Nchi jirani wa Kongo kama vile Burundi pia imekumbwa na mlipuko unaokua kwa Kasi, Ripoti ya WHO iliongeza.

Mpox inaweza kuenea kupitia mawasiliano ya karibu(Close contact). Inaweza kuonyesha dalili za Kawaida, lakini ni hatari na inaweza kusababisha Vifo katika hali za nadra.  Kwa kawaida husababisha dalili zinazofanana na mafua na vidonda vilivyojaa usaha mwilini.

#SOMA ZAIDI hapa Kuhusu Ugonjwa wa Mpox na Dalili Zake 

Taarifa ya WHO haikutoa takwimu linganishi za miaka iliyopita.

Shirika la afya ya umma la Umoja wa Afrika(The African Union’s public health agency) limesema visa 14,957 na vifo 739 viliripotiwa kutoka majimbo saba yaliyoathirika mwaka 2023 – Sawa na ongezeko la asilimia 78.5 la kesi mpya kutoka 2022.

 Kulikuwa na kesi 29,342 zinazoshukiwa na vifo 812 kote barani Afrika kuanzia Januari hadi katikati ya Septemba mwaka huu, kulingana na ripoti ya WHO.

 Jumla ya kesi 2,082 zilizothibitishwa ziliripotiwa kote ulimwenguni mnamo Agosti pekee, idadi kubwa zaidi tangu Novemba 2022.

 Siku ya Jumamosi, mfuko wa Benki ya Dunia wa janga la ugonjwa huu(World Bank’s pandemic fund) ulisema utatoa dola milioni 128.89 (euro milioni 115) kwa nchi kumi za Afrika kusaidia kupambana na mlipuko huo.

Reviewed via;

– Shirika la Afya Duniani(WHO)

– Reuters

– Shirika la afya ya umma la Umoja wa Afrika(The African Union’s public health agency) 

– https://www.rfi.fr/en/africa/20240924-who-reports-30-000-suspected-mpox-cases-in-africa-mainly-in-drc

-https://www.afyaclass.com/2024/09/ugonjwa-wa-homa-ya-nyanichanzodalili-na.html?m=1

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti9 hours ago

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50 Chanzo: CNN Health Mwandishi: Jacqueline Howard Tarehe: Novemba 12, 2026...

magonjwa ya watoto11 hours ago

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto,fahamu hapa

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto: Sababu, Dalili, Magonjwa Yanayoonekana Mara kwa Mara na Njia za Kuzuia Ngozi ni kiungo kikubwa...

Utafiti16 hours ago

Asilimia 63 ya Wauzaji wa Matunda Wanatumia Kemikali Kuchelewesha au Kuharakisha Kuiva kwa Ndizi na Nyanya

Wataalamu waonya kuhusu matumizi yasiyo sahihi ya kemikali katika kuiva kwa matunda, wakisema baadhi ya kemikali zinaweza kuwa na madhara...

WHO1 day ago

WHO yatoa Miongozo ya Kwanza ya Utambuzi na Udhibiti wa Kisukari cha Aina ya Kwanza kwa Watu Wazima

Shirika la Afya Duniani (World Health Organization – WHO) limetoa kwa mara ya kwanza miongozo ya kimataifa kuhusu utambuzi na...

magonjwa ya wanaume2 years ago

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo Tabia hii imekuwa ikiwaathiri Wanaume Wengi kwa hivi Sasa,Je unazifahamu athari au...

magonjwa1 day ago

HPV ni Ugonjwa gani?,Fahamu hapa

Human Papilloma Virus (HPV): Maana Yake, Magonjwa Inayosababisha Na Athari Zake Kwa Afya Human Papilloma Virus (HPV) ni nini? Human...

Hospital1 day ago

Waziri wa Afya,amewapongeza watumishi wanne kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto

Waziri wa Afya,amewapongeza watumishi wanne kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto Waziri wa Afya, Mohamed Omary Mchengerwa, amewapongeza watumishi...

Ebola2 days ago

Ugonjwa wa Ebola ulivyoleta Athari kwa watoto DRC

Ugonjwa wa Ebola ulivyoleta Athari kwa watoto DRC Kufikia tarehe 4 Novemba, watoto 2,959 wenye umri chini ya miaka 18...

magonjwa ya wanawake3 days ago

Madhara ya kuvurugika kwa homoni za kike (Hormonal Imbalance in women)

Kuvurugika kwa hormone au vichocheo ni nini? Kuvurugika kwa hormone au vichocheo hutokea pale mwili unapozalisha homoni kwa kiwango kikubwa...

Hospital4 days ago

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery)

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery) Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kuboresha huduma za kibingwa...