Connect with us

Events

Watoto wa kike milioni 5 nchini Tanzania kupatiwa chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi- WHO

Avatar photo

Published

on

Watoto wa kike milioni 5 nchini Tanzania kupatiwa chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi- WHO

#PICHA: Uzinduzi wa kampeni ya siku 5 ya kitaifa ya chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi nchini Tanzania uliambatana na wanawake na wanaume kubeba mabango yenye ujumbe kuhusu usalama wa chanjo hiyo.

Nchini Tanzania kampeni ya siku 5 ya chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, au Human Papilloma Virus, (HPV) imeingia siku ya tatu hii leo nchini kote ikilenga zaidi ya watoto wa kike milioni 5 wenye umri wa kati ya miaka 9 hadi 14.

Taarifa iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni huko jijini Geneva, nchini Uswisi na Mwanza nchini Tanzania inasema kampeni hiyo inaendeshwa kwa ubia kati ya serikali ya Tanzania,  Ubia wa chanjo duniani, GAVI , mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF na WHO.

Virusi vya HPV ni sababu kuu ya saratani ya shingo ya kizazi, kwingineko ikijulikana kama mlango wa kizazi au Cervical Cancer kwa lugha ya kiingereza na kampeni itamalizika tarehe 26 mwezi huu wa Aprili.

WHO inasema wakati saratani ya shingo ya kiazi inasalia kuwa moja ya sababu kuu ya vifo miongoni mwa wanawake nchini Tanzania, ambapo mwaka 2022 wagonjwa 6,800 kati ya 10,800 walifariki dunia, bado ugonjwa huo unazuilika kwa chanjo.

“Chanjo ya HPV ni salama na ina ufanisi mkubwa katika kuzuia maambukizi,” inasema WHO, ikiongeza kuwa wakati wa kampeni, watoto wa kike wenye umri wa kupatiwa chanjo hiyo watakuwa na fursa ya kupatiwa dozi moja ya chanjo bila gharama yoyote.

Muuguzi nchini Tanzania akimpatia mtoto wa kike chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, au HPV wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 5 ya chanjo hiyo kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Utoaji wa chanjo ya HPV Tanzania umekuwa wa mafanikio

Shirika hilo linaongeza kuwa juhudi za kuongeza upatikanaji wa chanjo hiyo dhidi ya saratani nchini kote Tanzania zimekuwa na mafanikio makubwa.

Mwaka 2018, chanjo hiyo inayotolewa kwa dozi mbili, ilijumuishwa kwenye programu ya chanjo ya kitaifa kwa watoto wote wa kike wenye umri wa miaka 14, ikionesha azma ya serikali ya Tanzania ya kulinda afya na ustawi wa vizazi vijavyo.

Hali leo hii, kwa mujibu wa WHO, ufikiaji wa dozi ya kwanza ya HPV ni asilimia 79, na dozi ya pili asilimia 60.

Ni kwa kuzingatia hilo, WHO inasema juhudi za pamoja zinahitajika kuhakikisha kila mtoto wa kike Tanzania anapata kinga hiyo muhimu dhidi ya ugonjwa huo hatari lakini wenye kinga.

Maendeleo ya Tanzania katika kutoa chanjo ya HPV ni muhimu kama sehemu ya mpango wa kimataifa unaoungwa mkono na Ushirika wa Chanjo ambao umeazimia kutoa fedha zaidi na rasilimali ili kuhakikisha watoto wa kike milioni 86 kote duniani wanakuwa wamepatiwa chanjo hiyo ifikapo mwaka 2025.

MASWALI&MAJIBU kuhusu afya| Link...👇

https://afyaclass.com/afyaforums

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa2 weeks ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa3 weeks ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa1 month ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa1 month ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa3 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake3 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa5 days ago

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu Haya ni maneno ambayo umekuwa ukiyasikia sana linapokuja swala la vipimo cha UKIMWI, je...

Magonjwa6 days ago

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia. Kutana na Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa unaosababishwa na konokono

Ugonjwa unaosababishwa na konokono Ugonjwa unaosababishwa na konokono unaitwa schistosomiasis, au bilharzia. Ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na minyoo wanaoitwa...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake. Wengi tumesikia kuhusu Red Eyes(Macho mekundu) Lakini je umewahi kusikia kuhusu Pink Eyes,?...

Magonjwa2 weeks ago

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapa

Omeprazole inatibu ugonjwa gani Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi...

Magonjwa2 weeks ago

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani Mate kujaa Mdomoni,ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na zipo...

Magonjwa2 weeks ago

Glaucoma: Ugonjwa hatari unaopoteza nuru ya macho

Glaucoma: Ugonjwa hatari unaopoteza nuru ya macho Kuna magonjwa mengi yanayohusiana na macho, mengi yanatibika lakini kuna baadhi ya magonjwa...

Magonjwa3 weeks ago

Kunguni husababisha ugonjwa gani

Kunguni husababisha ugonjwa gani Kunguni ni wadudu wadogo ambao chakula chao kikubwa ni damu, wadudu hawa huweza kunyonya damu kutoka...

Magonjwa4 weeks ago

je ugonjwa wa pumu unaambukiza

je ugonjwa wa pumu unaambukiza? Hili ni Swali ambalo watu wengi huuliza,hata kwenye page za afyaclass, kwa kuliona hilo, tumeona...

Magonjwa1 month ago

Dalili za mwanzo za ugonjwa wa ini

Dalili za mwanzo za ugonjwa wa ini Ugonjwa wa ini (hepatic disease) mara nyingi huanza taratibu na dalili zisizo wazi,...