Connect with us

WHO

WHO yataka huduma jumuishi za VVU na saratani ya shingo ya kizazi ili kuokoa maisha ya wanawake

Avatar

Published

on

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito wa kuimarishwa kwa huduma jumuishi za Virusi Vya Ukimwi na saratani ya shingo ya kizazi ili kuhakikisha wanawake na wasichana wanaoishi na magonjwa hayo wanapata huduma za kinga, uchunguzi, utambuzi na matibabu kwa wakati.

Wito huo umetolewa leo huko Geneva, Uswisi, ambayo ni Siku ya kimataifa ya Kutokomeza Saratani ya Shingo ya Kizazi, huku WHO ikionya kuwa wanawake wanaoishi na VVU wako katika hatari kubwa mara sita zaidi ya kupata saratani hiyo ikilinganishwa na wanawake wasio na VVU.

Licha ya changamoto hizo, juhudi za kimataifa za kukabiliana na ugonjwa huo zinaendelea kuimarika. WHO imesema zaidi ya asilimia 50 ya wasichana katika Kanda ya Afrika walipokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya virusi vya Human Papiloma, HPV mwaka 2025.

Aidha, takribani nchi 133 duniani zimeanzisha huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi.

WHO inasisitiza kuwa wanawake wanaoishi na VVU wanapaswa kupata huduma hizi kwa usawa, bila ubaguzi wala ucheleweshaji.

Malengo ya kimataifa ya 2030
WHO inalenga kutekeleza Mkakati wake wa Kimataifa wa malengo ya 90-70-90 ifikapo mwaka 2030. Haya yanajumuisha kuwapatia chanjo asilimia 90 ya wasichana dhidi ya HPV kabla ya umri wa miaka 15, kuwafanyia uchunguzi asilimia 70 ya wanawake kwa vipimo bora, na kuhakikisha asilimia 90 ya waliobainika kuwa na ugonjwa huo wanapata matibabu na huduma stahiki.

Mkurugenzi wa Idara ya VVU, Kifua Kikuu, Homa ya Ini na Maambukizi ya Zinaa wa WHO, Dkt Tereza Kasaeva, amesema kuunganisha huduma za VVU na saratani kutasaidia kupunguza vifo na kuboresha maisha ya wanawake.

Hakuna mwanamke anayeachwa nyuma
WHO pia inashirikiana na Shirika lake tanzu la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC) kuchunguza uwezekano wa kujumuisha HPV35 katika chanjo za baadaye.

Shirika hilo linasisitiza kuwa hali ya mtu ya kuishi na VVU haipaswi kamwe kuwa kikwazo cha kupata huduma za saratani kwa wakati. Lengo ni kuhakikisha kila mwanamke na msichana anapata huduma bora bila kuachwa nyuma.

Source:UN

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

afyatips6 hours ago

Vyakula vya kuongeza damu Tanzania

Tanzania kuna vyakula vingi vinavyoweza kusaidia kuongeza damu mwilini, hasa vile vyenye madini ya Iron (chuma), ambayo mwili hutumia kutengeneza...

Afya News7 hours ago

Wizara ya Afya yakemea Imani POTOFU dhidi ya Mabusha/ngirimaji

WIZARA YA AFYA YAKEMEA IMANI POTOFU DHIDI YA MABUSHA/NGIRIMAJI Na Alex Nkondo, WAF – Handeni, Tanga Wataalamu wa afya wanaohudumu...

WHO9 hours ago

WHO yataka huduma jumuishi za VVU na saratani ya shingo ya kizazi ili kuokoa maisha ya wanawake

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito wa kuimarishwa kwa huduma jumuishi za Virusi Vya Ukimwi na saratani ya shingo...

Utafiti1 day ago

Muunganisho kati ya mama na mtoto huendelea hata baada ya ujauzito,Maternal Microchimerism

Muunganisho kati ya mama na mtoto huendelea hata baada ya ujauzito,Maternal Microchimerism Muunganisho kati ya mama na mtoto wake unaenda...

Utafiti2 days ago

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50 Chanzo: CNN Health Mwandishi: Jacqueline Howard Tarehe: Novemba 12, 2026...

magonjwa ya watoto2 days ago

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto,fahamu hapa

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto: Sababu, Dalili, Magonjwa Yanayoonekana Mara kwa Mara na Njia za Kuzuia Ngozi ni kiungo kikubwa...

Afya News2 days ago

Huduma ya Kutomtenganisha Mama na Mtoto Njiti kupunguza VIFO kwa asilimia 25

Huduma ya Kutomtenganisha Mama na Mtoto Njiti kupunguza VIFO kwa asilimia 25 Na Shaban Juma, WAF – Dar es Salaam...

Utafiti2 days ago

Asilimia 63 ya Wauzaji wa Matunda Wanatumia Kemikali Kuchelewesha au Kuharakisha Kuiva kwa Ndizi na Nyanya

Wataalamu waonya kuhusu matumizi yasiyo sahihi ya kemikali katika kuiva kwa matunda, wakisema baadhi ya kemikali zinaweza kuwa na madhara...

WHO3 days ago

WHO yatoa Miongozo ya Kwanza ya Utambuzi na Udhibiti wa Kisukari cha Aina ya Kwanza kwa Watu Wazima

Shirika la Afya Duniani (World Health Organization – WHO) limetoa kwa mara ya kwanza miongozo ya kimataifa kuhusu utambuzi na...

magonjwa ya wanaume2 years ago

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo Tabia hii imekuwa ikiwaathiri Wanaume Wengi kwa hivi Sasa,Je unazifahamu athari au...