Connect with us

Afya News

Wizara ya Afya yakemea Imani POTOFU dhidi ya Mabusha/ngirimaji

Avatar

Published

on

WIZARA YA AFYA YAKEMEA IMANI POTOFU DHIDI YA MABUSHA/NGIRIMAJI

Na Alex Nkondo, WAF – Handeni, Tanga

Wataalamu wa afya wanaohudumu katika kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya mabusha/ngirimaji wameendelea kutoa huduma kwa wananchi huku wakisisitiza umuhimu wa usafi wa mazingira, kujikinga na mbu pamoja na kuachana na imani potofu zinazohusishwa na ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa leo, Novemba 18, 2026, wilayani Handeni, mkoani Tanga, na Mratibu wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele wa Wilaya ya Handeni, Dkt. Clarence Mangowi, wakati akizungumzia maendeleo ya kambi hiyo na umuhimu wa wananchi kuchukua hatua za kujikinga dhidi ya magonjwa hayo.

Dkt. Mangowi amesema utunzaji wa mazingira, hususan kuondoa mazalia ya mbu na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi, ni hatua muhimu katika kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa matende unaoweza kusababisha mabusha/ngirimaji.

Aidha, amewataka wananchi kuachana na imani potofu zinazohusisha ugonjwa wa mabusha na masuala ya kishirikina, akieleza kuwa ugonjwa huo unaweza kuchunguzwa na kutibiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kulingana na chanzo chake.

Amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza katika kambi hiyo ili kupata huduma za uchunguzi, ushauri wa kitaalamu na matibabu stahiki, badala ya kuficha hali zao au kuchelewa kutafuta huduma kutokana na hofu, unyanyapaa na taarifa zisizo sahihi.

Dkt. Mangowi amewahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na wataalamu wa afya, kuzingatia usafi wa mazingira na kutumia fursa ya huduma zinazotolewa katika kambi hiyo ili kupunguza madhara ya mabusha/ngirimaji na kuboresha afya na ustawi wa jamii.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

afyatips6 hours ago

Vyakula vya kuongeza damu Tanzania

Tanzania kuna vyakula vingi vinavyoweza kusaidia kuongeza damu mwilini, hasa vile vyenye madini ya Iron (chuma), ambayo mwili hutumia kutengeneza...

Afya News7 hours ago

Wizara ya Afya yakemea Imani POTOFU dhidi ya Mabusha/ngirimaji

WIZARA YA AFYA YAKEMEA IMANI POTOFU DHIDI YA MABUSHA/NGIRIMAJI Na Alex Nkondo, WAF – Handeni, Tanga Wataalamu wa afya wanaohudumu...

WHO9 hours ago

WHO yataka huduma jumuishi za VVU na saratani ya shingo ya kizazi ili kuokoa maisha ya wanawake

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito wa kuimarishwa kwa huduma jumuishi za Virusi Vya Ukimwi na saratani ya shingo...

Utafiti1 day ago

Muunganisho kati ya mama na mtoto huendelea hata baada ya ujauzito,Maternal Microchimerism

Muunganisho kati ya mama na mtoto huendelea hata baada ya ujauzito,Maternal Microchimerism Muunganisho kati ya mama na mtoto wake unaenda...

Utafiti2 days ago

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50 Chanzo: CNN Health Mwandishi: Jacqueline Howard Tarehe: Novemba 12, 2026...

magonjwa ya watoto2 days ago

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto,fahamu hapa

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto: Sababu, Dalili, Magonjwa Yanayoonekana Mara kwa Mara na Njia za Kuzuia Ngozi ni kiungo kikubwa...

Afya News2 days ago

Huduma ya Kutomtenganisha Mama na Mtoto Njiti kupunguza VIFO kwa asilimia 25

Huduma ya Kutomtenganisha Mama na Mtoto Njiti kupunguza VIFO kwa asilimia 25 Na Shaban Juma, WAF – Dar es Salaam...

Utafiti2 days ago

Asilimia 63 ya Wauzaji wa Matunda Wanatumia Kemikali Kuchelewesha au Kuharakisha Kuiva kwa Ndizi na Nyanya

Wataalamu waonya kuhusu matumizi yasiyo sahihi ya kemikali katika kuiva kwa matunda, wakisema baadhi ya kemikali zinaweza kuwa na madhara...

WHO3 days ago

WHO yatoa Miongozo ya Kwanza ya Utambuzi na Udhibiti wa Kisukari cha Aina ya Kwanza kwa Watu Wazima

Shirika la Afya Duniani (World Health Organization – WHO) limetoa kwa mara ya kwanza miongozo ya kimataifa kuhusu utambuzi na...

magonjwa ya wanaume2 years ago

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo Tabia hii imekuwa ikiwaathiri Wanaume Wengi kwa hivi Sasa,Je unazifahamu athari au...