Magonjwa
MUDA WA KUMEZA DAWA PAMOJA NA MAELEKEZO YAKE
MUDA WA KUMEZA DAWA PAMOJA NA MAELEKEZO YAKE
Kwa hivi sasa watu wengi wamekuwa wakitumia dawa pasipo kuzingatia matumizi sahihi ya muda kwenye Dawa husika.
Tatizo ambalo huweza kusababisha mtu kujioverdose Dawa bila yeye kujua.
Mfano: Utakutana na mtu anasema yeye kaambiwa ameze dawa asubuh na jion, au kutwa mara tatu, hivo anameza asubuh mchana na jion,
bila kujua asubuh na jion ni masaa mangapi au kutwa mara tatu ni masaa mangapi toka kumeza dawa.
NB: Kwa kuliona hilo, Leo nimeamua kukuandalia makala hii ambayo itakufungua macho, na kukusaidia kuzingatia muda sahihi kwenye matumizi ya dawa ulizopewa.
Pia itakusaidia wewe kuepuka kujioverdose dawa,badala yake utatumia dawa kwenye kiwango sahihi pamoja na muda sahihi unaotakiwa.
MUDA WA KUMEZA DAWA PAMOJA NA MAELEKEZO YAKE
1. Ukiambiwa dawa hizi meza kutwa MARA TATU au kwa kitaalam unaweza andikiwa kwa kifupi “tds”
– Maana yake unatakiwa kumeza dawa hizi KILA BAADA YA MASAA 8.
hivo kutwa mara tatu sio asubuh, mchana na jion tu, no ila ni kila baada ya masaa 8.
2. Ukiambiwa dawa hizi meza kutwa MARA MBILI, Haina maana ya asubuh na jion tu
– Bali,maana yake unatakiwa kumeza dawa hizi KILA BAADA YA MASAA 12.
3. Ukiambiwa dawa hizi meza kutwa MARA MOJA, au kwa kitaalam unaweza andikiwa kwa kifupi “OD” Ikiwa na maana ya ONCE PER DAY.
– Maana yake unatakiwa kumeza dawa hizi KILA BAADA YA MASAA 24.
mfano: kama umemeza dawa leo saa moja kamili asubuh ni mpaka kesho saa moja kamili asubuhi(hayo ndyo masaa 24).
Nimatumaini yangu kwamba umeelewa matumizi sahihi ya MUDA kwenye dawa ulizopewa.
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
-
Uzazi/Ujauzito5 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Magonjwa4 days ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Uzazi/Ujauzito3 days ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
Magonjwa7 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Magonjwa2 days ago
kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani
-
Events6 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
News4 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani
-
Utafiti23 hours ago
Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHO