Magonjwa
UNAWEZA KUPATA UGONJWA WA BRUCELLA KWA KULA NYAMA AMBAYO HAIJAPIKWA VIZURI PAMOJA NA MAZIWA AMBAYO HAYAJACHEMSHWA VIZURI
UNAWEZA KUPATA UGONJWA WA BRUCELLA KWA KULA NYAMA AMBAYO HAIJAPIKWA VIZURI PAMOJA NA MAZIWA AMBAYO HAYAJACHEMSHWA VIZURI
Ugonjwa wa Brucella ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Brucellosis na chanzo chake kikubwa ni maambukizi ya Bacteria wanaojulikana kama BRUCELLA,
Bacteria hawa hutoka kwa wanyama mbali mbali kama vile; Ng’ombe, mbuzi,kondoo,Nguruwe,Mbwa n.k, na kwa hivi sasa watu wengi hupatwa na ugonjwa wa Brucella ambao hupimwa kupitia kipimo cha damu,
DALILI ZA UGONJWA WA BRUCELLA
fahamu kuhusu dalili mbali mbali za ugonjwa wa Brucella, kwa kusoma baadhi ya dalili hizo hapa chini;
1. Mgonjwa kupatwa na homa ambazo hujirudia mara kwa mara
2. Mgonjwa kuhisi kama vile kuna vitu vinatembea mwilini mwake, na wakati mwingine huhisi kama minyoo wakati wa kujisaidia haja kubwa
3. Mgonjwa kuanza kutetemeka mwili baada ya kuhisi baridi kali
4. Mgonjwa kupoteza kabsa hamu ya kula chakula au kitu chochote
5. Mgonjwa kutoa jasho kupita kiasi
6. Mwili kuchoka sana pamoja na kuwa dhaifu
7. Mgonjwa Kupata maumivu ya joints,misuli pamoja na maumivu ya mgongo
8. Mgonjwa Kupata maumivu ya kichwa mara kwa mara
9. Pia mgonjwa huweza kupatwa na tatizo la kuvimba kwa kuta za ndani ya chemba za moyo yaani endocarditis
10. Mgonjwa kupatwa na tatizo la kuvimba kwa joints pamoja na mifupa ya uti wa mgongo yaani spinal bones, tatizo ambalo hujulikana kwa kitaalam kama Spondylitis.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
-
Uzazi/Ujauzito5 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Magonjwa4 days ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Uzazi/Ujauzito3 days ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
Magonjwa7 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Magonjwa2 days ago
kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani
-
Events6 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
News4 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani
-
Utafiti22 hours ago
Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHO