Connect with us

News

Tanzania miongoni mwa nchi 5 kutokomeza ukimwi ifikapo 2030

Avatar photo

Published

on

Tanzania miongoni mwa nchi 5 kutokomeza ukimwi ifikapo 2030

Dunia iko mbioni kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030 mara tu programu muhimu za afya zitakapofadhiliwa kikamilifu, ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema.

Eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako asilimia 65 ya watu wote wenye VVU wanaishi pia linapiga hatua kubwa katika kutokomeza ugonjwa huo.

Botswana, Eswatini, Rwanda, Tanzania na Zimbabwe tayari zimefikia lengo la ’95-95-95′, kwa mujibu wa UNAIDS.

Hii ina maana 95% ya watu wanaoishi na VVU wanajua hali zao za VVU, 95% ya watu wanaojua hali zao wanapata matibabu ya kurefusha maisha, na 95% ya watu wanaopata matibabu wamevifubaza virusi hivyo, na hivyo haiwezekani. kusambaza.

Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amezungumza na mwandishi wa BBC Roncliffe Odit na ameanza kwa kuelezea ufanisi huu umetokana na nini hasa.

Mataifa mengine 16, nane kati yao katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara pia yanakaribia kufikia lengo hili.

“Mwisho wa Ukimwi ni fursa ya urithi wenye nguvu ya kipekee kwa viongozi wa leo,” Winnie Byanyima, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, katika taarifa yake.

“Wanaweza kuokoa mamilioni ya maisha na kulinda afya ya kila mtu. Wanaweza kuonesha kile ambacho uongozi unaweza kufanya.”

Lakini UNAIDS inakabiliwa na upungufu wa dola bilioni 8.5 katika bajeti yake kwa nchi za kipato cha chini na cha kati ifikapo mwaka 2025.

Inasema maendeleo yanaweza kuharibiwa kwa urahisi ambapo mtu mmoja alikufa kila dakika kutokana na Ukimwi mwaka 2022.

“Ukweli na takwimu zilizoshirikiwa katika ripoti hii hazioneshi kuwa kama ulimwengu tayari tuko njiani, zinaonesha kuwa tunaweza kuwa,” alisema Bi Byanyima. “Njia iko wazi.”

Wasichana walio hatarini

Lakini bado kuna vikwazo vya kushinda. Kila wiki, wasichana na wanawake 4,000 wanaambukizwa VVU.

Na katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, licha ya maendeleo, Umoja wa Mataifa unasema wanawake na wasichana wa rika zote walichangia asilimia 63 ya maambukizi mapya ya VVU mwaka 2022.

Jaribio la chanjo ya VVU linaendelea nchini Uganda, Tanzania na Afrika Kusini ambalo linachanganya chanjo za majaribio za VVU na pre-exposure prophylaxis (PrEP) kwa wakati mmoja, jambo ambalo halijawahi kufanywa hapo awali.

Nchini Botswana kusini mwa Afrika, wasichana wanasalia katika hatari ambapo wanaume wazee huwawinda, inayojulikana kama ‘ngono kati ya vizazi’.

Gaone ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 ambaye aliambukizwa VVU akiwa msichana wa shule.

“Mmoja wa ndugu zangu wa karibu sana alikuwa akinisaidia sana, alikuwa na umri wa miaka thelathini, mara mbili ya umri wangu, nilimwamini, alinitumia vibaya na kufanya mapenzi na mimi,” anasema.

Gaone amekuwa akitumia dawa za kurefusha maisha tangu 2012 na ni mama wa watoto wawili. Watoto wake wawili hawana VVU na sasa anafanya kazi kama mwanakampeni.

Anasema jamii haiko tayari kuzungumza waziwazi kuhusu ‘ubakaji’ na ‘unyonyaji wa kingono’.

“Katika baadhi ya siku, ninapokea jumbe kutoka kwa wanawake wengi kama watano waliopata VVU kutoka kwa wazee, wengi wao wakiwa jamaa zao. Ikiwa wanaume hawatasikiliza, tunaweza kufanya nini?” anauliza.

Nguvu ya maombi

Takwimu zote zinaonesha wanaume walioambukizwa VVU wanasitasita zaidi kuliko wanawake kutafuta msaada wa matibabu.

Botswana sasa inahusisha viongozi wa imani kujaribu kubadilisha mitazamo ya wanaume na kuzuia maambukizi ya VVU.

“Nchini Botswana, asilimia 95 ya watu wenye VVU wanajua hali zao. Wengi wao ambao hawajui hali zao ni wanaume,” anasema Mchungaji Mmachakga Mpho Moruakgomo, kiongozi wa Kikristo ambaye ni sehemu ya kundi la madhehebu mbalimbali linaloshughulikia suala hilo. .

“Kwa kuwa watu wanaheshimu viongozi wa imani, tunaitumia kuzungumza na wanaume kuhusu haja ya kupima na kujiandikisha kupata matibabu mara tu hali zao zitakapothibitishwa.”

Kasisi Moruakgomo anasema viongozi wa Kiislamu, Hindu na Bahai pamoja na waganga wa kienyeji wanahusika na wengine hata kwenda nyumba kwa nyumba kueneza ujumbe huo.

Kampeni hiyo inaitwa ‘Ndugu Amkeni – Nanogang’, iliyochochewa na maneno kutoka kwa wimbo wa taifa wa nchi hiyo.

“Kuna unyanyapaa mwingi kuhusu VVU. Sisi viongozi wa imani tuliwajibika kwa hilo,” mchungaji wa Kanisa la African Methodist Episcopal Church anakiri waziwazi.

“Tulihukumu sana na kuwalaumu wale walioambukizwa. Ngono na ujinsia ni msingi kwa maisha yetu. Tunahitaji kuomba msamaha na kukiri kwamba tulikosea.”

Ontiretse Letlhare, mkuu wa Shirika la Kitaifa la masuala ya Ukimwi na Afya (NAPHA). anasema Botswana iko njiani kuumaliza Ukimwi ifikapo mwaka 2030 na ina matumaini viongozi wa kidini wanaweza kutoa msukumo huo muhimu.

“Suala muhimu ni kuongeza juhudi za kuondoa unyanyapaa wa VVU na kuepuka hali ambapo watu wanaoishi na VVU wanaweza kuogopa kutafuta huduma za VVU kutoka kwenye vituo vya afya.”

Mwenendo huo sio chanya katika ulimwengu wote ambapo Umoja wa Mataifa unasema karibu robo moja ya maambukizi mapya ya VVU yalikuwa Asia na Pasifiki mnamo 2022.

Ongezeko kubwa la maambukizi mapya linaendelea katika Ulaya mashariki na Asia ya kati (kupanda kwa 49% tangu 2010) na Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (ongezeko la 61% tangu 2010).

Inasema mwelekeo huu unatokana na ukosefu wa huduma za kuzuia VVU kwa watu waliotengwa na sheria ambazo zinafanya jumuiya ya LGBTQ+ kuwa ya jinai.

Lakini matibabu yanayojulikana kama pre-exposure prophylaxis au PrEP yanatoa matumaini.

Kambodia katika Asia Mashariki inatoa vidonge hivi bila malipo kwa watu walio katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara ya ngono, mashoga na jumuiya ya watu waliobadili jinsia.

Ulimwengu wote

Mwenendo huo sio chanya katika ulimwengu wote ambapo Umoja wa Mataifa unasema karibu robo moja ya maambukizo mapya ya VVU yalikuwa Asia na Pasifiki mnamo 2022.

Ongezeko kubwa la maambukizi mapya linaendelea katika Ulaya mashariki na Asia ya kati (kupanda kwa 49% tangu 2010) na Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (ongezeko la 61% tangu 2010).

Inasema mwelekeo huu unatokana na ukosefu wa huduma za kuzuia VVU kwa watu waliotengwa na sheria ambazo zinafanya jumuiya ya LGBTQ+ kuwa ya jinai.

Lakini matibabu yanayojulikana kama pre-exposure prophylaxis au PrEP yanatoa matumaini.

Kambodia katika Asia Mashariki inatoa vidonge hivi bila malipo kwa watu walio katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara ya ngono, mashoga na jumuiya ya watu waliobadili jinsia.

Tembe ya kila siku ina dawa zinazotumika kutibu VVU na ni ya kuzuia pale ambapo mtu hana VVU kwa kuanzia.

“Ninatumia vidonge mara kwa mara kwa miezi mitatu. Siku chache za kwanza, niliumwa na kichwa lakini hakukuwa na madhara mengine. Ninakunywa kidonge kwa siku,” anasema Kuy Pov, mwanamke aliyebadili jinsia mwenye umri wa miaka 32 ambaye anamiliki. saluni katika mji mkuu Phnom Penh.

“Ninatumia PrEP, kwa sababu nina wapenzi wengi wa ngono. Najua niko hatarini,” akiongeza kuwa huwa anawauliza wapenzi wake kuvaa kondomu lakini wakati mwingine wanakataa.

Cambodia ina wastani wa watu 76,000 wanaoishi na VVU. Asilimia themanini na sita ya watu hawa, zaidi ya wanne kati ya watu watano, wanajua hali zao. Na kati ya hao, karibu 99% wanaweza kupata matibabu.

Maambukizi mapya yamepungua kwa 91% ikilinganishwa na 1996. Lakini takribani watu wanne wanaambukizwa kila siku ambayo inabakia kuwa wasiwasi mkubwa.

“Hapo awali matumizi ya kondomu yalikuzwa, lakini kulikuwa na wengi ambao hawakutumia.

PrEP ni njia bunifu ya kusaidia jamii katika kuzuia maambukizi ya VVU,” anasema Danou Chy, ambaye anafanya kazi katika shirika lisilo la kiserikali la Men’s Health. Cambodia, katika mji mkuu.

Vidonge vya PrEP vinatoa matokeo ya kutia moyo, anasema, na kuna mipango ya kuanzisha toleo la sindano.

Matibabu mapya yamempa Kuy udhibiti wa sehemu muhimu ya maisha yake.

Hivi karibuni alipima VVU na alifurahi kujua hana.

Source: Bbc

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa2 months ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa3 months ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa3 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa3 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa5 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake5 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa4 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa2 days ago

kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani

kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani Unapopata tatizo la kuharisha na kutapika kwa wakati mmoja unaweza kuwaza sana,...

Magonjwa4 days ago

Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu

Dalili za infection kwenye damu Mchafuko wa damu,chanzo,dalili na Tiba Mchafuko wa damu; hiki ni kiswahili ambacho watu wamezoea kukitumia...

Magonjwa7 days ago

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri Yapo magonjwa mbali mbali ya ngozi ambayo huweza kuathiri Sehemu za Siri za Mwanaume...

Magonjwa2 weeks ago

Dalili za acid reflux,Soma hapa Kufahamu

Dalili za acid reflux: Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), ni tatizo ambalo huwapata Watu wengi,Tatizo hili hujulikana kwa jina...

Magonjwa4 weeks ago

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe au ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi kupoteza rangi...

Magonjwa4 weeks ago

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu Baada ya Ugonjwa huu wa macho kusumbua watu wengi kwa kipindi cha Hivi Karibuni,...

Magonjwa1 month ago

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu Utangulizi: Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo...

Magonjwa1 month ago

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume Gono ni neno maarufu ambalo kirefu chake ni Gonorrhea na kiswahili chake ni...

Magonjwa1 month ago

Dalili Mpya za ukimwi kwenye ngozi

Zipi ni Dalili za ukimwi kwenye ngozi Zipi ni dalili za Ukimwi kwenye ngozi ya mtu? Fahamu hapa kupitia makala...

Magonjwa1 month ago

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu Huu ni ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na kirusi cha corona, ambao...

Trending