News
Rais wa Namibia Hage Geingob amefariki dunia leo
Rais wa Namibia Hage Geingob amefariki dunia leo Feb 04,2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Lady Pohamba iliyopo Mji Mkuu wa Nchi hiyo Windhoek.
Ofisi ya Rais wa Namibia imethibitisha taarifa hiyo na kusema amefariki wakati Mkewe Monica Geingos na Mwanae wakiwa karibu nae.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 82 aligunduliwa kuwa anaugua saratani na alitangaza hali yake mbele ya umma mwezi uliopita na baadaye ofisi yake ilitangaza kwamba atasafiri kuelekea Marekani kupata matibabu, itakumbukwa pia alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka jana, na mwaka 2014 alitangaza kuwa amepona saratani ya tezi dume.
Geingob aliapishwa kuwa Rais mwaka 2015 na alikuwa anatumikia awamu yake ya pili na ya mwisho ya uongozi.
-
Uzazi/Ujauzito5 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Magonjwa4 days ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Uzazi/Ujauzito3 days ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
Magonjwa7 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Magonjwa2 days ago
kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani
-
Events6 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
News4 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani
-
Utafiti21 hours ago
Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHO