Magonjwa
MAUMIVU YA TUMBO AMBAYO HUSHUKA MPAKA KWENYE MIGUU
MAUMIVU YA TUMBO AMBAYO HUSHUKA MPAKA KWENYE MIGUU
Unaweza kupata maumivu ambayo huanzia tumboni,eneo la sehemu za siri,kiunoni mpaka kwenye mguu mmoja wa kulia,kushoto au miguu yote miwili.
CHANZO CHA MAUMIVU KAMA HAYA
– Ujauzito, baadhi ya wanawake wajawazito hupata Maumivu haya ambayo huanzia tumboni mpaka miguuni,
Hii ni kutokana na Ujauzito kusababisha pressure zaidi kwenye misuli,ligaments za eneo la kiunoni(pelvis) kuvutwa zaidi n.k
Na maumivu haya huweza kuwa makali hasa wakati mama mjamzito akitembea.
Ukiwa unapata maumivu kama haya unaweza kuomba ushauri kutoka kwa wataalam wa afya wakuambie nini chakufanya.
– Tatizo la Fibromyalgia, Tatizo hili huhusisha maumivu makali sana na ya muda mrefu ambayo husambaa mpaka kwenye misuli, Maumivu haya huambatana na;
• Uchovu wa mwili kupita kiasi
• Maumivu kwenye viungo,joints pamoja na misuli
• Kushindwa kufocus kwenye kitu unachokifanya
• Kuwa na shida ya Depression
• Kukosa usingizi
• Kupata maumivu makali ya kichwa
• Kuwa na hofu au wasi wasi sana
• Kuhisi vitu vinachoma choma kwenye mikono pamoja na miguuni
• Tumbo kujaa gesi,Kupata choo kigumu
• Maumivu ya tumbo,uso,taya n.k
KUMBUKA; ukiwa na tatizo hili kuna dawa pamoja na vitu vya kufanya ukiwa nyumbani ikiwemo mazoezi ya kukusaidia hilo tatizo likaisha kabsa.
– Tatizo la Pelvic floor dysfunction, tatizo hili huweza kusababishwa na ujauzito,umri mkubwa,kuumia kama kuchanika sana wakati wa kujifungua n.k
Japo kwa asilimia kubwa ya wanawake wenye tatizo hili hawapati maumivu yoyote ila hupata shida ya kushindwa kuzuia mkojo kutoka hasa wakati wa kukimbia au kuruka.
Matibabu yake huweza kuhusisha dawa pamoja na mazoezi ila kama tatizo ni kubwa sana yaani severe pelvic floor injuries basi hapa lazima upasuaji kufanyika.
– Tatizo la Sciatica pain, ambalo huhusisha maumivu makali kuanzia nyuma ya mgongo(lower back) na kusambaa kwenye maeneo mengine mpaka miguuni,
Na chanzo chake ni shida kwenye sciatic nerve, ambapo husababishwa na vitu mbali mbali kama vile; Kuharibiwa kwa Nerves hizo, maumivu yanayotokana na ugonjwa wa kisukari yaani diabetic nerve pain,tatizo la herniated disc n.k
– Tatizo la Myofascial pain syndrome, haya ni maumivu makali ambayo huanzia sehemu moja kama kwenye kifundo cha msuli mgumu, kisha kusambaa kwenye maeneo mengine mwilini,
Maumivu haya huweza kutibiwa kwa dawa, mfano wa jamii ya steroids, muscle relaxants,n.k, Pamoja na Massage na mazoezi.
– Tatizo la Soft tissue injuries, hapa nazungumzia ligaments, tendons au muscles ambazo huzunguka eneo la pelvis kwa wanawake.
Endapo soft tissue kwenye maeneo haya zikapata jeraha lolote, huweza kusababisha maumivu kwenye eneo la kiuno,hips, tumboni kushuka chini sehemu za siri ambayo husambaa hadi miguuni.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
-
Uzazi/Ujauzito5 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Magonjwa4 days ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Uzazi/Ujauzito3 days ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
Magonjwa7 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Magonjwa2 days ago
kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani
-
Events6 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
News4 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani
-
Utafiti21 hours ago
Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHO