News
Umuhimu wa papai katika mlo wako,Hakikisha haukosi
Umuhimu wa papai katika mlo wako,Hakikisha haukosi
Kama ulikuwa hujui, jifunze sasa, papai ni tunda lililo na vitamini C kwa wingi pamoja na vitamini A.
Papai ni tunda lenye radha nzuri mdomoni, lakini ni chanzo kizuri cha asidi ya foliki ambayo huimarisha mfumo wa fahamu, hasa watoto, pindi mimba inapotungwa.
Kama ulikuwa hujui, jifunze sasa, papai ni tunda lililo na vitamini C kwa wingi pamoja na vitamini A.
Ofisa Mtafiti Mwandamizi wa Sayansi na Chakula, kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe( TFNC), Francis Modaha amesema
vitamini C iliyopo katika papai, huimarisha kuta za mishipa ya damu, fizi na huondoa viini haribifu mwilini.
Amesema vitamini A iliyopo kwa wingi katika papai, huimarisha kinga mwili, uoni, ngozi, ukuaji mzuri wa mtoto na maendeleo mazuri kwa watoto wadogo.
Papai pia, lina vitamini B1, 2, 5, E na K na kwamba uwepo wa vitamini K husaidia ufyonzaji wa madini ya chokaa mwilini, hivyo huchangia kuimarisha mifupa.
Modaha amesema papai husaidia umeng’enyaji wa chakula kwa sababu lina vimeng’enyo.
Mtaalamu huyo wa lishe amesema uwepo wa kimeng’enyo kwenye tunda la papai bichi hutumika mara nyingi kulainisha nyama.
Modaha amesisitiza kuwa ulaji wa papai mara kwa mara husaidia kupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kutokana na uwepo wa vitamini na madini mbalimbali katika tunda hilo.
-
Uzazi/Ujauzito5 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Magonjwa4 days ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Uzazi/Ujauzito3 days ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
Magonjwa7 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Magonjwa2 days ago
kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani
-
Events6 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
News4 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani
-
Utafiti22 hours ago
Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHO