Connect with us

News

Je, kuna athari za kiafya kuchoma sindano ya kuzuia mikunjo usoni?

Avatar photo

Published

on

Je, kuna athari za kiafya kuchoma sindano ya kuzuia mikunjo usoni?

Sindano ya Botox ni maarufu na kwa kiasi kikubwa ni salama kutumia. Lakini inaelezwa inaweza kuleta athari kwa matumizi ya muda mrefu. Botox ni biashara kubwa.

Botox (botulinum neurotoxin) ni dawa ya sindano maarufu zaidi kwa urembo wa kuondoa mikunjo usoni. Takribani sindano milioni tatu zinazokadiriwa kutumika kila mwaka.

Inafanya kazi ya kuzuia ishara ya mikunjo. Matokeo yake ni kuwa na uso wa ujana – kwa takribani miezi mitatu hadi minne.

Inatazamwa kama sindano salama, yenye ufanisi na isiyo na madhara makubwa. Lakini, je ni salama kweli? Madhara mengi yaliyoripotiwa ni madogo na ya muda mfupi.

Ni pamoja na maumivu, uvimbe au michubuko kidogo kwenye eneo ilipopita sindano, na maumivu ya kichwa. Pia kuna dalili kama za mafua kwa saa 24 za kwanza na mwili kulegea kwa muda.

Lakini kuna athari mbaya zaidi zimetokea. Mwezi Aprili 2024, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekanni (CDC) kilitoa onyo kwamba wanawake 22 wa umri wa miaka 25 na 59 wameripoti hivi karibuni athari mbaya za Botox.

Watu 11 walilazwa hospitalini, na sita walitibiwa kutokana na wasiwasi wa huenda kuna sumu katika mfumo mkuu wa neva na ambayo inaweza kusababisha kupooza kwa misuli, ugumu wa kupumua, na hata kifo.

Dalili zilizoripotiwa ni pamoja na kutoona vizuri na kuona vitu viwili viwili, kope zinazolegea, ugumu wa kumeza, ugumu wa kuzungumza, kupumua kwa shida, uchovu, na udhaifu.

Kesi zote 22 zilitokea baada ya wanawake hao kuchoma sindano za Botox kutoka kwa watu wasio na leseni au wasio na mafunzo katika maeneo ambayo hayakuwa na mazingira ya huduma za afya.

“CDC, FDA (Kitengo cha kudhibiti Dawa), na watu wa mamlaka wanachunguza magonjwa haya ambayo yalitokea baada ya watu kudungwa vibaya au kudungwa sindano feki,” anasema Michelle Waltenburg, mtaalamu wa magonjwa katika kutoka CDC.

Athari mbaya kiasi gani?

“Sumu ya botulinum ikitengenezwa vizuri na kwa usahi, nguvu yake hata ikisambaa kidogo haileti madhara makubwa,” anasema Ash Mosahebi, profesa wa upasuaji wa urembo kutoka Chuo Kikuu cha College London.

“Kiasi cha sumu iliyomo hakiwezi kuwapa watu ugonjwa wa botulism (kupooza misuli, ugumu wa kupumua ama kifo). Hata hivyo, tatizo ambalo tumekuwa nalo ni kwamba kuna matoleo ghushi yanayosambazwa ya sindano hiyo. Hayajatengenezwa vizuri, na hayadhibitiwi vyema.”

Kwa hivyo Botox bandia ni habari mbaya. Lakini vipi kuhusu usalama wa Botox ya kawaida? Utafiti wa 2020 ulikagua usalama wa sindano za vipodozi za Botox, na kuhitimisha kuwa ripoti za athari mbaya kama zile zilizoonekana na CDC ni nadra.

Kwa mfano, kati ya 2002-03 ni athari mbaya ya sindano hiyo ni kesi 36 pekee ndizo ziliripotiwa kwa FDA, na nyingi zikihusu ugumu wa kumeza.

Hatari ya athari mbaya ilikuwa mara 33 zaidi kwa matumizi mengine ya Botox kuliko yale matumizi kwa ajili ya vipodozi (Botox wakati mwingine hutumiwa kutibu kipandauso, mshtuko wa shingo, jasho, mikojo kupita kiasi, jicho kupunguza nusu na hali zingine).

Lakini inawezekana kuwa athari mbaya haziripotiwi. Utafiti wa 2023 uliofanywa na Mosahebi na wenzake katika chuo kikuu cha UCL uligundua 69% ya waliohojiwa walipata athari mbaya za muda mrefu, kama vile maumivu, wasiwasi na maumivu ya kichwa kutoka na Botox. Pia kulikuwa na athari kubwa za kisaikolojia na kihisia kwa wagonjwa pale matibabu yanapokwenda vibaya.

“Ikiwa itafanyika vibaya inaweza kulegeza kope zako, na hiyo kudumu kwa miezi sita,” anasema Mosahebi

Madhara ya muda mrefu

Kuna taarifa kidogo sana kuhusu madhara ya muda mrefu. Hata hivyo baadhi ya tafiti zimegundua kuwa matumizi ya muda mrefu yanaweza kusababisha mabadiliko ya kudumu katika sura, na watu kushindwa kukunja misuli yao ya uso.

Utafiti wa 2022 uligundua watu ambao waliochomwa sindano za Botox mara kwa mara walionyesha mabadiliko katika muundo wa misuli yao, utendajikazi wa misuli na mwonekano kwa miaka minne baada ya sindano yao ya mwisho.

Kuna ushahidi kwamba matumizi ya muda mrefu ya Botox yanaweza kuwa na athari za kisaikolojia kwa wagonjwa.

Katika utafiti wa 2023, Mitchell Brin, daktari wa neva katika Chuo Kikuu cha California, Irvine, na wenzake walichunguza akili za wanawake 10 kabla na baada ya kupokea sindano za Botox.

Kwenye uchunguzi wa baada ya sindano ya Botox, wanawake walionyesha hisia kubadilika katika maeneo mawili ya ubongo yanayojulikana kuwa na jukumu la kuchakata hisia.

Hii inalingana na matokeo ya tafiti zingine, ambazo zimeonyesha kuwa kuchoma sindano za Botox kunaweza kuifanya iwe ngumu kutambua na kuelewa hisia za mtumiaji.

Kwa mfano, tunapoona jambo la furaha au huzuni kwa wengine, tutumia misuli yetu ya uso kujenga hisia. Hii hutusaidia kuelewa na kufasiri jinsi wengine wanavyohisi.

Lakini kwa sababu Botox inapooza misuli ya uso, hatuwezi tena kuwa na uso wa hisia kwa wengine, na hivyo basi kutufanya tuonekane hatuna huruma.

Kipi cha kufanya?

Kwanza, watu wanaotumia sindano za Botox wachome kutoka kwa watoa huduma walio na leseni ambao wamefunzwa, na wanaelewa mpangilio wa huduma ya afya.

Watengenezaji wa Botox, walisema katika taarifa kwa BBC kwamba watumiaji wanapaswa kuhakikisha wanapitia kwa mtaalamu wa matibabu aliyeidhinishwa.

Msemaji wa kampuni hiyo aliongeza: “Kipaumbele chetu ni afya na usalama wa wagonjwa na ripoti zote za bidhaa ghushi zinachunguzwa kwa kina na timu yetu na kwa kushirikiana na vyombo vya sheria na udhibiti.

Hivi karibuni Mosahebi alifanya uchanganuzi wa sindano za vipodozi nchini Uingereza, na kugundua 68% ya wataalamu wa urembo wanaotoa sindano kama vile Botox sio madaktari .

Lakini ikiwa inasimamiwa kwa usahihi, kuna kila sababu ya kufikiria kuwa Botox ni salama kwa kiasi kikubwa. Inatumika sana, na ina sifa ya kuwa salama,” anasema Meunier.

“Kumekuwa na baadhi ya watu ambao wamepata athari mbaya, lakini unapaswa kuliweka hilo katika muktadha wa mamilioni ya watu ambao wametumia sindano hii tangu miaka ya 1980 na 90 bila madhara.” Via:BBC

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa2 months ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa3 months ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa3 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa3 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa4 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake5 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa7 hours ago

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri Yapo magonjwa mbali mbali ya ngozi ambayo huweza kuathiri Sehemu za Siri za Mwanaume...

Magonjwa4 days ago

Dalili za acid reflux,Soma hapa Kufahamu

Dalili za acid reflux: Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), ni tatizo ambalo huwapata Watu wengi,Tatizo hili hujulikana kwa jina...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe au ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi kupoteza rangi...

Magonjwa3 weeks ago

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu Baada ya Ugonjwa huu wa macho kusumbua watu wengi kwa kipindi cha Hivi Karibuni,...

Magonjwa3 weeks ago

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu Utangulizi: Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo...

Magonjwa4 weeks ago

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume Gono ni neno maarufu ambalo kirefu chake ni Gonorrhea na kiswahili chake ni...

Magonjwa4 weeks ago

Dalili Mpya za ukimwi kwenye ngozi

Zipi ni Dalili za ukimwi kwenye ngozi Zipi ni dalili za Ukimwi kwenye ngozi ya mtu? Fahamu hapa kupitia makala...

Magonjwa1 month ago

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu Huu ni ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na kirusi cha corona, ambao...

Magonjwa1 month ago

Ishara za Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) kwa Wanaume na Wanawake

Ishara za Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) kwa Wanaume na Wanawake Karibu! Hapa kwa makala yenye taarifa muhimu kuhusu...

Magonjwa1 month ago

Vyanzo Vya Kifo cha Ghafla: Sababu Zinazotisha na Jinsi ya Kujikinga

“Vyanzo Vya Kifo cha Ghafla: Sababu Zinazotisha na Jinsi ya Kujikinga” Kifo cha ghafla ni janga lisilotarajiwa ambalo linaweza kumpata...

Trending