News
MADHARA YATOKANAYO NA UVAAJI WA SURUALI ZA KUBANA
SURUALI ZA KUBANA
• • • • • •
MADHARA YATOKANAYO NA UVAAJI WA SURUALI ZA KUBANA
Watu wengi wamekuwa wakivaa suruali za kubana sana hasa hasa wakina dada,bila kujua pia uvaaji wa suruali za kubana sana una madhara kiafya.
Swala la kuvaa suruali za kubana sana mapaja kwa wadada au wanawake imekuwa fashion kwa watu wengi, na huku baadhi yao wakifikia hatua ya kutokuwa na Nguo nyingine zaidi ya suruali tu.
YAPI NI MADHARA YA KUVAA SURUALI ZA KUBANA SANA?
– Wataalam wa afya wanasema uvaaji wa suruali za kubana sana mapaja ya mtumiaji kwa muda mrefu husababisha tatizo la kukandamiza mshipa wa fahamu ambao hupita eneo la mapajani ambao kwa kitaalam hujulikana kama Lateral femoral cutaneous nerve.
Madhara ya Mgandamizo huu wa mshipa wa fahamu unaopita kwenye eneo la paja la Mtu ni kupata ganzi pamoja na kupata tatizo la kuhisi kuchomwa chomwa kwenye eneo la paja ambapo tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama Tingling thigh syndrome au Meralgia paresthetica.
USHAURI
• Wataalam wa afya wanapendekeza mtu kuvaa nguo ambazo haziubani sana mwili wake ikiwa ni pamoja na kuacha kabsa tabia ya kuvaa suruali za kubana sana mapaja pamoja na kuvaa viatu virefu sana kwa Muda mrefu.
Kwa kudokeza tu kwa ufupi Madhara ya Uvaaji wa Viatu virefu ni pamoja na;
– kupata maumivu makali ya kiuno na mgongo
– kupata maumivu ya miguu kwenye joint
– kudondoka
– Kupata tatizo la misuli ya mwili kukaza
N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
-
Uzazi/Ujauzito6 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Uzazi/Ujauzito4 days ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
Magonjwa5 days ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Magonjwa3 days ago
kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani
-
Events7 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
News5 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani
-
afyatips21 hours ago
Madhara ya damu kuwa nyingi mwilini
-
Utafiti2 days ago
Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHO