Magonjwa
DALILI ZA UTI SUGU KWA MWANAMKE NA MWANAUME NI ZIPI?
UTI SUGU
_______________
DALILI ZA UTI SUGU KWA MWANAMKE NA MWANAUME NI ZIPI?
Kwanza tujue tukisema UTI tuna maana gani na tukisema UTI Sugu tuna Maana gani. Pamoja na tofauti zake ni zipi
• Kwa ufupi UTI kirefu chake ni Urinary track Infection na maana yake ni maambukizi katika mfumo mzima wa Mkojo ukijumuisha maeneo mbali mbali kama vile; kibofu cha Mkojo(urinary bladder), Njia ya mkojo(urethra), Figo, pamoja na tezi mbali mbali kama Prostate gland.
Maambukizi haya kwa asilimia kubwa huwa ya Bacteria,ambapo yanaweza kuwa ya mda mfupi,ya mda mrefu,au ya kujirudia rudia mara kwa mara.
• UTI SUGU maana yake; ni maambukizi katika mfumo mzima wa mkojo ambayo yamekuwa ya kujirudia rudia kila mara na ya mda mrefu hata baaada ya kutumia dawa nyingi na matibabu mbali mbali.
DALILI ZA UTI KWA WOTE(MWANAMKE NA MWANAUME) NI PAMOJA NA;
- Kupata maumivu makali ya nyonga,mgongo,joint pamoja na viungo mbali mbali vya mwili
- Kupata maumivu ya tumbo hasa hasa upande wa kushoto
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara ila ukikojoa mkojo haushi
- Kuhisi hali ya kuchoma wakati wa kukojoa
- Kukojoa mkojo wenye rangi kama pink au nyekundu,hii ni baada ya UTI kuwa ya mda mrefu na kuanza kuleta madhara makubwa
- Kuhisi hali ya uume kuwaka Moto
- Kuhisi hali ya kuchoma au kuwasha kwenye tundu au njia ya mkojo
- Kupata uchovu wa mwili kupita kiasi au Mwili kuchoka sana
- Joto la mwili kuwa juu au Mtu kuwa na Homa(Fever)N.k
MADHARA YA UTI SUGU
Uti ikishakuwa ya mda mrefu huweza kuleta madhara makubwa kama;
– Matatizo ya Figo
– Kwa mwanamke kuwa hali ya Uke Mkavu kupita kawaida
– Shida kwenye kibofu cha Mkojo
– N.K
MATIBABU YA UTI
Zipo dawa mbali mbali Nzuri kwa ajili ya Kutibu kabsa tatizo la UTI, Ila ni vizuri kufanya Vipimo kwanza ili kujua hali ya tatizo lako au;
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
KUMBUKA PIA: Zingatia Kunywa Maji mengi kila siku angalau Lita 2.5 mpaka 3, kwani maji husaidia pia kwa Kiwango kikubwa,
Zipo baadhi ya Tafiti zinaonyesha unywaji wa Maji mengi angalau lita 2.5 kwa siku huweza kupunguza hatari ya wewe kupata UTI kwa zaidi ya asilimia 50%, Hivo Maji ni muhimu Pia kwako.
-
Uzazi/Ujauzito5 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Magonjwa4 days ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Uzazi/Ujauzito3 days ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
Magonjwa7 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Magonjwa2 days ago
kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani
-
Events6 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
News4 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani
-
Utafiti23 hours ago
Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHO