Magonjwa
USHAURI KWA MWANAMKE BAADA YA MIMBA KUTOKA(miscarriage)
MIMBA
• • • • •
USHAURI KWA MWANAMKE BAADA YA MIMBA KUTOKA
Tatizo la mimba kutoka zenyewe yaani Miscarriage hutokea sana kwa wanawake wengi kwa hivi sasa,
Na asilimia kubwa ya mimba huharibika kwenye miezi mitatu(3) ya mwanzoni yaani First trimester
Je baada ya mimba kutoka,ni mambo gani mwanamke anatakiwa kuzingatia?
BAADHI YA MAMBO YA KUZINGATIA KWA MWANAMKE BAADA YA UJAUZITO KUHARIBIKA
– Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kupumzika
– Epuka kufanya kazi nzito na za kunyanyua vitu vizito
– Hakikisha unapata vyakula ambavyo vinakiwango cha kutosha cha madini ya Chuma yaani Iron-rich foods
– Hakikisha unapata virutubisho vyenye aina zote za Vitamins kwa kiwango kikubwa Yaani Multivitamins
– Matumizi ya dawa ambazo umepewa hospital kwa ajili ya kukukinga na kupata maambukizi ya magonjwa mbali mbali ni muhimu sana Mfano; dawa jamii ya Antibiotics
– Ni vizuri kutokufanya mapenzi mpaka damu iache kutoka, ambapo kwa wataalam wa afya hushauri angalau ukae hata kipindi cha Wiki 6 bila kufanya mapenzi
– Kaa kwa muda mrefu kidogo kabla ya kubeba ujauzito mwingine, angalau kwa kipindi cha Miezi sita(6) na kuendelea
– Usitumie vitu mbali mbali wakati unaosha sehemu zako za siri, wala usiweke vidole sehemu zako za siri
N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
-
Uzazi/Ujauzito5 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Magonjwa4 days ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Uzazi/Ujauzito3 days ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
Magonjwa7 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Magonjwa2 days ago
kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani
-
Events6 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
News4 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani
-
Utafiti22 hours ago
Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHO