Events
Mvulana mwenye Kifafa awa Wakwanza Duniani kuwekewa Kifaa kwenye Fuvu Lake
![](https://afyaclass.com/mk_omb/uploads/2024/06/fd607190-31e6-11ef-903f-61734aec5b6f.jpg.webp)
Mvulana mwenye Kifafa awa Wakwanza Duniani kuwekewa Kifaa kwenye Fuvu Lake.
Mvulana aliye na kifafa kikali amekuwa mgonjwa wa kwanza duniani kujaribu kifaa kipya kilichowekwa kwenye fuvu la kichwa ili kudhibiti mshtuko.
Kichochezi cha neva, ambacho hutuma ishara za umeme ndani ya ubongo wake, kimepunguza mshtuko wa Oran Knowlson kwa 80%.
Mama yake, Justine, aliiambia BBC kuwa alikuwa na furaha zaidi na alikuwa na “maisha bora zaidi”.
Upasuaji huo ulifanyika Oktoba mwaka jana kama sehemu ya majaribio katika Hospitali ya Great Ormond Street huko London wakati Oran, ambaye sasa ana umri wa miaka 13 alikuwa na umri wa miaka 12.
Oran, kutoka Somerset, ana ugonjwa uitwao kitaalamu Lennox-Gastaut, aina ya kifafa sugu ambacho kilianza akiwa na umri wa miaka mitatu.
Tangu wakati huo amekumbwa na mshtuko wa moyo mara kadhaa kila siku.
Tulipozungumza kwa mara ya kwanza na mama yake Oran majira ya vuli mwaka jana, kabla ya upasuaji, alieleza jinsi kifafa cha Oran kilivyotawala maisha yake: “Kimempokonya utoto wake wote.”
Alituambia Oran alikuwa na aina mbalimbali za kifafa, ikiwa ni pamoja na vile ambapo alianguka chini, akatetemeka kwa nguvu, na kupoteza fahamu.
Alisema wakati fulani alikuwa akiacha kupumua na kuhitaji dawa za dharura ili kupata pumzi yake tena.
Oran ana usonji na ADHD, lakini Justine anasema kifafa chake ndicho kikwazo kikubwa zaidi: “Nilikuwa na mtoto mchanga mwenye umri wa miaka mitatu, na ndani ya miezi michache baada ya kushikwa na kifafa alidhoofika haraka, na kupoteza uwezo wake mwingi. “
-
Magonjwa4 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Uzazi/Ujauzito2 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Elimu&Ushauri6 days ago
Afya za watu bilioni 1.8 duniani matatani kwa kutokufanya Mazoezi – WHO
-
Magonjwa1 day ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Events3 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
Uzazi/Ujauzito11 hours ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
News6 days ago
Mlipuko Mbaya wa homa ya nyani watokea tena KIVU KASKAZINI
-
News2 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani