Dawa
WHO yatoa orodha mpya ya bakteria sugu dhidi ya dawa
![](https://afyaclass.com/mk_omb/uploads/2024/05/image350x235cropped-4.jpg)
WHO yatoa orodha mpya ya bakteria sugu dhidi ya dawa
Shirika la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa.
Katika taarifa iliyotolewa leo, WHO inafafanua kuwa usugu wa vijiumbemaradhi dhidi ya dawa hutokea pale ambapo bakteria, virusi, fangasi, na vimelea vingine vya magonjwa haviitikii tena dawa, hivyo kuongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa, watu kuugua na hata vifo.
WHO inaeleza kwamba kwa sehemu kubwa hali hii ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa inasababishwa na matumizi mabaya ya dawa za viuavijumbe maradhi.
Utafiti huu mpya uliotolewa leo unajumuisha uthibitisho mpya na maarifa ya kitaalamu ili kuongoza utafiti na maendeleo kwa ajili ya viuavijiumbemardahi yaani Antibiotics mpya na kuhamasisha uratibu wa kimataifa ili kukuza uvumbuzi.
Baadhi ya bakteria sugu zilizotajwa ni Neisseria gonorrhoeae inayosababisha na Mycobacterium tuberculosis inayosababisha ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).
Orodha kama hii ya vijiumbemaradhi hatari kwa afya ya binadamu ambavyo vimejenga usugu dhidi ya dawa, ilitolewa na WHO miaka 7 iliyopita.
-
Magonjwa4 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Elimu&Ushauri6 days ago
Afya za watu bilioni 1.8 duniani matatani kwa kutokufanya Mazoezi – WHO
-
Uzazi/Ujauzito2 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Magonjwa1 day ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Events3 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
Uzazi/Ujauzito10 hours ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
News6 days ago
Mlipuko Mbaya wa homa ya nyani watokea tena KIVU KASKAZINI
-
News2 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani